JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................429-430
Sura ya: 429
Kisha, Sarah aliinamisha kichwa chake na kuachia kicheko kidogo.
Hakutarajia Maya kuwa mwanamke wa Master Ganja. Hilo lilimvutia sana.
Ikiwa kweli Alvin asingerudi kwake, asingejali kumwangamiza mtu ambaye angeweza kumchukua.
Lakini, sasa haukuwa wakati wake.
Alipompigia tena Rodney, sauti yake ilikuwa laini. "Rodney, unafanya nini?"
"Sarah, namsubiri Pamela." Sauti ya Rodney ilisikika. "Sasa, ni Pamela pekee anayeweza kunisaidia kuiokoa Osher, kwa hivyo ninahitaji kumrudisha mwanamke huyo kwenye kampuni."
Damu ya Sarah ilichemka baada ya kumsikia. Moyo wa Alvin ulikuwa umetekwa na Lisa. Halafu sasa, hata mpango wake wa kando, Rodney alikuwa akimzungukia Pamela siku nzima.
Kwa kweli alihisikama dunia nzima imepanga kumfanyia njama!
"Rodney, nina hasira sana." Sarah alisikika akiwa na huzuni. "Nilikuwa na Maya, lakini sasa, pia amehamishwa."
"Si amekuwa akikulinda muda wote huu?" Sauti ya Rodney ililipuka ghafla.
"Anafuata tu maagizo ya ONA." Sarah akahema kwa uchungu. “Mlezi aliondoka pia, akisema nina hasira. Kwa kweli sikutarajia kwamba ningeishia katika hali hii.”
"F*ck. Alvin ni mjinga. ” Rodney hakutarajia Alvin angekuwa hana moyo kiasi hicho. Hata kama alitaka kuachana naye, je, ilimbidi awe na kinyongo hivyo na kuwahamisha wafanyakazi wake? “Usifikirie juu yake. Nitakuja mara moja.”
Hata hivyo, alipokata simu na kugeuka ili kuondoka, alimuona Pamela akiwa amesimama nyuma yake. Hakujua ni muda gani yeye alikuwa amesimama hapo.
Alikuwa amevalia vazi jeupe lililofumwa na kofia nyeupe ya baseball kichwani. Kwa tabasamu hafifu kwenye kona ya mdomo wake, alionekana mrembo na asiyeeleweka mwanzoni.
"Hi, Mwenyekiti Shangwe. Ulijuaje kuwa nimehamia Brighton Gardens?" Pamela alitabasamu. "Bwana Kimaro alikuambia?"
Rodney alikasirika sana baada ya kutajwa kwa Alvin.
Chester ndiye aliyemwambia. Alikumbuka kuwa hii ni nyumba ya Alvin, lakini aliihamishia kwa Pamela.
Pamela alihema kwa nguvu. “Alvin ni mkarimu kupita kiasi. Nilitaka kubaki na Lisa, lakini alihisi kwamba nilikuwa ninawaendesha kwa gurudumu la tatu, kwa hiyo akanipa ghorofa hii. Kuishi hapa peke yangu ni nraha sana. ”…
“Umemaliza?” Akiwa njia kumfuata Pamela, Rodney alijiambia kudhibiti hasira yake. Hata hivyo, aligundua kwamba kila alipowasiliana na mwanamke huyu, shinikizo la damu lilipanda. Hakutaka kitu zaidi ya kumkata vipande vipande.
“Hakika. Nimemaliza. Unaondoka?” Pamela alimtazama kimya kimya.
“…Ndio. naondoka.” Rodney alichanganyikiwa aliposema. Alikuwa amemngoja kwa muda mrefu sana, lakini alipotokea, alikuwa kishamuahidi Sara kwamba angeenda.
“Bwana Shangwe, umepofushwa sana na upendo.” Pamela alivutiwa. “Ili tu kumuwahi Sarah, hata hujali kuhusu kampuni yako. Ikiwa hutafanya kazi kwa bidii, naweza kushirikiana na SE Group katika siku chache zijazo. Bila kutaja, nina fomula mpya niliyotengeneza mkononi mwangu. Matokeo ni mazuri sana, na malighafi sio ghali. Bwana Malugu anaitaka vibaya sana.”
Rodney alifikiria juu ya jambo fulani, na alikuwa karibu kuzungumza wakati Pamela alipogeuka na kuanza kuondoka.
“Subiri…” Aliongea kwa haraka.
"Nini? Si unaondoka? Si unamuwahi Sarah?” Pamela aliuliza kwa mshangao.
Rodney aliona aibu. Je, angewezaje bado kuwa katika hali ya kumuona Sarah? “Pamela Masanja, tuongee. ”
“Kuongea? Hakuna cha kuzungumza. Kila unapozungumza na mimi, unakasirika na kuanza kupiga kelele. Kwa hivyo, sina muda wa kubishana na wewe.” Pamela alipunga mkono kwa uso wa kikauzu.
Uso mzuri wa Rodney ulikunjamana kwa hasira. Jamani. Alifanya ionekane kana kwamba ni kosa lake. Yeye ndiye aliyemkasirisha. Kwa kawaida alikuwa muungwana sana kwa wanawake wengine.
“Pamela, najua kwamba nilienda mbali sana hapo awali, lakini unajua kuwa wale wanawake wabaya ulionipambanisha nao mara ya mwisho... Umeniharibia jina?!”
"Unasema nini? Unapaswa kunishukuru. Kama si mimi, wazazi wako wangekulazimisha kumuoa yule binti usiyemtaka. Lakini sasa, kwa sababu yangu, hakuna mtu ambaye yuko tayari kuchumbiwa nawe, kwa hivyo unaweza kuendelea kumngoja Sarah Njau wako. Siyo nzuri hii?”
Pamela alijibu mara moja, na sentensi 'Nilifanya hivi kwa faida yako mwenyewe' iliandikwa kwenye uso wake wa fahari.
Rodney kwa mara nyingine akashusha pumzi ndefu. “Sawa, asante. Wewe ni mfadhili wangu. Je, ninaweza kukununulia chakula cha jioni, mfadhili?”
Pamela akatikisa kichwa. “Sitaki kwenda nje. Nimekuwa nikila chakula cha nje kila siku, na tumbo langu halijisikii vizuri, kwa hiyo nataka kula chakula cha kupika mwenyewe. Unaweza kunipikia?”
"Nini?" Rodney alifikiri alikuwa kiziwi.
“Hutaki? Ikiwa hutaki, basi usahau. Nilifikiri tunaweza kutumia nafasi hii ili tuongee juu yake…”
“Sawa, nitafanya.” Rodney alijikaza kiume na kumfuata. Hakuwahi kufikiria kuwa ingetokea siku ambayo ingebidi asikilize mihemko ya Pamela.
Baada ya kupanda ghorofani, Pamela alijitupa kwenye sofa. Kisha, akararua vitafunio kwenye meza na kuanza kula. “Fanya haraka kupika. Ikiwa chakula kitakuwa kibaya, basi hakuna nafasi ya kuzungumza. Pia, usifikirie hata kumwomba mtu msaada. Mimi ni aina ya mtu ambaye anapenda uaminifu."
Rodney alifungua jokofu kwa uso uliojaa huzuni. Kulikuwa na vitu vingi ndani, lakini ilikuwa tu mtindi, maziwa fresh, na matunda. Hakukuwa na vyakula vya kupikia. Baada ya kutafuta kwa muda mrefu, aliona nyama na samaki waliogandishwa kwenye friji. Aliangalia tarehe. Zinge expire ndani ya muda wa siku mbili.
Alinyamaza kimya akimtazama yule mwanamke aliyekuwa nje na hakujua ni mwanamke wa aina gani. Hakika hakuwa mwanamke mwema, na hakuna mtu aliyetaka mwanamke kama huyo.
Pamela aliingia baada ya kula pakiti ya chips za viazi na kumuona akipunguza baridi ya nyama hiyo. Alikuwa ameipika hapo awali alipoinunua tu. Hata hivyo, kwa kuwa nyama hiyo haikuungwa, ilikuwa na ladha mbaya sana.
Ndani ilikuwa mbichi pia.
“Unatengeneza nyama? Hiyo ni ngumu kupika." Kutokana na wema wa moyo wake, Pamela alimkumbusha, “Kwanini usishuke chini ukanunue mboga ili kupika chakula chepesi tu?”
"Hakuna haja." Rodney alimtazama kwa huzuni.
Uso wake ulimfanya Pamela amfikirie mbwa wake huko Dar es Salaam.
Kisha, akageuka na kumpigia mama yake simu ya video. “Mama, Milo yuko wapi? Nilimwona mvulana anayefanana na Milo na nikamkumbuka ghafla.
“Mwanaume gani?” Mama yake alicheka huku akileta mbwa mdogo wa hudhurungi haraka. "Lazima aonekane wa ajabu sana ikiwa anafanana na Milo mdogo. Haahaahaaa."
“Si ajabu. Yeye ni kama msichana."
"Oh, unazungumza juu ya wanaume wa kike? Binti mjinga, ukitafuta mchumba, utafute wa kiume. Usiendelee kukaa peke yako. Unapaswa kuanza kuniletea wajukuu.”
Huko jikoni, Rodney alijichukia kwa kusikia maneno hayo. Alimwona mtu aliyefanana na mbwa? Mwanaume huyo alikuwa kama msichana? Alikuwa effeminate? Dume-Jike? Rodney alikuwa na uhakika wa 100% kwamba Pamela alikuwa akimzungumzia yeye. Hili lilikuwa tusi kwake.
Akajikaza sana jikoni na kushusha pumzi ndefu. Alilazimika kuvumilia.
Baada ya kuzungumza na mama yake kwa zaidi ya dakika 40, harufu nzuri ilikuja kutoka jikoni, na akakata simu ya video.
Muda si muda, Rodney alitoka na sahani za nyama, Ugali na samaki wa kukaanga.
Pamela alipigwa na butwaa. “Sh*t. Unaweza kupika kweli?" Macho yalimtoka kana kwamba ameona mzimu.
Sura ya: 430
Rodney aliuma meno. “Inabidi ushangae hivyo? Je, ni ajabu kwamba naweza kupika?”
“Ndio. Machoni mwangu, wewe ni bwana mdogo asiye na faida, mwenye kudekezwa ambaye hujui kufanya lolote zaidi ya kufuata maagizo ya Sarah na kufanya matakwa yake kila siku.” Pamela alitikisa kichwa bila kusita.
Rodney alichukia sana. Alipaswa kuweka sumu kwenye sahani mapema ili kumaliza yote.
Pamela alikata kipande kidogo cha nyama na kuonja. ladha ilikuwa ya kushangaza ... nzuri sana. Ilikuwa na ladha ya kweli kama nyama iliyopikwa na mama yake. Ugali ulikuwa laini na hata samaki walikaangwa vizuri.
"Hivi umetengeneza wewe mwenyewe?" Alikuwa na hamu ya kutaka kujua. "Hukuomba wasaidizi wako kuituma kupitia kwa dirisha la jikoni kwa drone?"
"Hapana, nilifanikiwa mwenyewe. Nilipenda kupika tangu nilipokuwa mdogo, sawa?" Rodney alishindwa kuvumilia.
“Hii ni kweli ni ajabu. Kupika kwa Alvin ni majanga, kwa hivyo sikuwahi kufikiria kuwa angekuwa na rafiki kama wewe. ” Pamela akahema tena. Ilikuwa ni mara ya kwanza kumtazama kwa makini Rodney.
Sifa za mtu huyo zilikuwa nzuri, na macho yake yalionekana kama yanaweza kumshawishi mtu wakati wowote. Umbo lake jembamba lilipendeza katika mavazi yoyote. Ikiwa angejiunga na tasnia ya burudani, bila shaka angekuwa aina vijana ambayo wanawake huwa waanapagawa nao.
“Mbona unanishangaa hivyo? Mimi nakuambia, sitaanguka kwa ajili yako.” Rodney alijisikia vibaya chini ya macho yake na akasema haraka, "Tunaweza kuzungumza juu ya formula sasa?"
“Hakika. Endelea." Pamela akaitikia kwa kichwa.
"Rodney alisema, "Ninajua unataka kushirikiana na SE Group, lakini ni lazima nikukumbushe kwamba SE daima imekuwa chini ya Osher kwa huduma ya ngozi nchini. Kawaida huwalenga wanafunzi. Wanawake wa tabaka la juu wanaidharau bidhaa zao. Ukifanya nao kazi, utakuwa unashusha hadhi yako.
"Pili, SE Group ina maduka machache kuliko sisi, iwe ya ndani au nje ya nchi. Ukichagua Osher Corporation, bidhaa zako zitakuwa na nafasi ya kuwa maarufu nchini kote na nchi jirani. Lakini ukichagua SE, inaweza kuuzwa tu nchini Kenya kwa wingi. Kando na hilo, Mwenyekiti wa SE Group, Lincoln Malugu, ni bahili na mkatili hata kwa mtoto wake mwenyewe Bwana Erick Malugu.”
"Kama wewe, ni mkatili na huna huruma pia." Pamela alidhihaki.
Rodney alijizatiti na kusema, “Lincoln Malugu ana tabia ya kuhonga wanawake. Anatupa pesa kwa wanawake wa nje lakini hatoi hata senti moja kwa mkewe nyumbani. Niamini. Yeye ni tajiri sana, lakini kijana wake Erick Malugu amesoma kwa shida sana. Mkewe na binti yake mdogo bado wanaishi katika nyumba ya vyumba viwili.. Mara tu kashfa hii ikizuka, itakuwa pigo kubwa kwa SE.
Baada ya yote, SE inapata pesa kutoka kwa wanawake.
"Je, huogopi kwamba nitamwambia Bwana Malugu?" Pamela aliinua macho yake.
“Tayari nimetuma ushahidi wote kuhusiana na ulaghai wake kwa mkewe. Labda atafanya tukio hivi karibuni." Rodney alikata nyama yake polepole na kwa utaratibu huku akisema, "Hata kama mke wake hatatoa ushirikiano, nina uwezo wa kulikuza mimi mwenyewe."
"Nakuamini. Nani asiyejua kuwa Alvinarah Media Network ya Kimaro inamiliki nusu ya vyombo vya habari vya mtandaoni nchini humu?” Pamela alicheka. "Bwana Shangwe, inaonekana kama nilikudharau."
“Hapana, hukunidharau. Umeikadiria SE Group kupita kiasi." Rodney alitikisa kichwa.“ Bidhaa zilizosalia za SE hazitoshi kushindana na Osher. Ingawa tumekuwa na migongano mingi isiyopendeza hapo awali, wewe ni mtu mwerevu, Bi.
Masanja. Kwanini ufanye mambo yawe magumu kwa pesa na kazi yako?"
Pamela alidhihaki. “Kama nisingepigana sana, maisha yangu ya baadaye yangeharibiwa na nyinyi. Rodney Shangwe, uliza dhamiri yako. Umewahi kujisikia hatia kuhusu mimi?
“Kwako, mimi nilikuwa ni mwanakemia wa kawaida wa vipodozi. Lakini je, umewahi kufikiria jinsi tnilivyojitahidi kupambana kwa ajili ya kampuni yako? Wakati ninyi mlipokuwa mkinywa pombe na kucheza na marafiki zako, nilikuwa bado nachoma mafuta ya usiku wa manane kwenye maabara. Ulipotoka kucheza mpira na kwenda kuvua samaki, nilibaki nyumbani tukipiga vitabu.” Macho ya Pamela hayakuweza kujizuia kuwa mekundu alipokuwa akiongea.
"Unaelewa jinsi ulivyonikatisha tamaa wakati ulinifukuza na kuniblacklist? Tukio la Thomas Njau lilitokea kwa bahati mbaya wakati huo huo, na niliharibiwa kabisa sifa yangu. Sikuweza kupata kazi na sikuweza kukubalika popote, kwa hiyo nililazimika kwenda ng’ambo.
"Kama mgeni, nilidharauliwa hadi nje ya nchi. Sikurudi hata kwenye nyumba yangu kila siku. Kati ya siku 365 kwa mwaka, nilitumia siku 350 kukesha katika maabara na kuzirai mara kadhaa.
"Kuna mara mbili nililala kwenye sakafu baridi usiku kucha na niliamka peke yangu kwenda hospitalini. Nilifikiria kukata tamaa, lakini nilijipa moyo na kupigana ili nirudishe hali yangu ya kujistahi iliyopotea.”
Kadiri alivyozidi kuwaza jambo hilo ndivyo moyo wake ulivyozidi kuwa mchungu, machozi yakimtoka.
"Halo, usilie." Rodney alijisikia hatia kidogo alipokuwa akimsikiliza, akashindwa kumuona akilia. Alimfanya ajione kama kweli alikuwa na hatia.
"Nina huzuni na kuumia, lakini hauniruhusu nilie." Machozi ya Pamela yalianguka chini kwa matone makubwa.
Hata hivyo, kulikuwa na msemo usemao kwamba mtu akiwa mrembo anaonekana mrembo zaidi akiwa analia. Ilikuwa ni kama matone ya mvua yakianguka kwenye petals za maua.
"Sawa, endelea kulia." Rodney alinyamaza kimya kutokana na kukemea
Kwake.
"Rodney Shangwe, wewe ni mwanaume? Ninalia, lakini bado hujui jinsi ya kunifariji. Si ajabu huwezi kupata rafiki wa kike.” Pamela akamrushia kitambaa alichokuwa ametumia kujifuta machozi.
"Pamela Masanja, unakosa akili kidogo." Rodney alikasirika.
"Wanawake siku zote hawana akili." Pamela akamfonza. Uso wake uliojaa machozi maridadi, mdogo na mzuri sasa ulikuwa mzuri sana kuutazama.
Kumtazama, Rodney kwa namna fulani alifikiri kwamba ngozi yake ilikuwa nzuri sana, na kwa kweli alionekana mzuri kidogo baada ya kulia.
“Nimefikiria. Tunaweza kushirikiana.” Pamela ghafla alisema, "Fomula ni dola laki 5 kila moja. Wakati huo huo, ninataka pia asilimia 10 ya hisa za Osher Corporation. Kila mwaka, Osher italazimika kuwekeza dola milioni 40 katika kutengeneza bidhaa mpya. Zaidi ya hayo, ninataka kuhudumu kama mkurugenzi wa idara ya R&D (maendeleo na utafiti) ya Osher.”
Rodney alishtuka. "Masharti mengine ni sawa, lakini unataka asilimia 10 ya hisa? Huo ni wizi wa mchana.”
“Fikiria jambo hilo. Usiposhirikiana nami, bado nitachagua SE. Hata kama SE inakumbwa na kashfa hasi, mimi natafuta pesa tu. Zaidi ya hayo, unapaswa kuelewa nguvu zangu. Mkemia wa vipodozi mwenye kipawa kama mimi anaweza kugunduliwa lakini hatafutwi. Ikiwa utaichukua nafasi hii au la itategemea wewe.”
Pamela akapangusa pua yake na kuanza kula nyama hiyo kwa raha zake.
Muonekano huo ulimfanya Rodney ashuku kuwa kilio chake hapo awali kilikuwa ni uzushi tu.
Rodney aliondoka baada ya chakula cha jioni, lakini masharti ya Pamela bado yalikuwa akilini mwake. Kwa hivyo, jambo la kwanza alilofanya ni kuelekea kwenye kampuni kwa mkutano.
Ilipofika saa 11 jioni Sarah alipiga simu, ndipo alipokumbuka kuwa alikuwa amesahau kumtembelea Sarah hospitalini.
“Samahani, Sarah. Nimekuwa busy na mikutano. sikukusudia.”.....ITAENDELEA..
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
