JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................407-408
Sura ya: 407
Baada ya kimya cha dakika nzima, Mzee Shangwe alipiga meza kwa furaha. "Anachukulia pesa kama uchafu? Hakika ninamfanya Pamela Masanja kuwa mke wa mjukuu wangu. Apende asipende.”
Jason alikasirika, lakini Wendy alikuwa makini zaidi. “Alvin alikuwa amemshika Lisa mkono mapema. Hiyo ina maana gani? Je, wanarudiana tena? Si ataomuoa Sara?”
“Hawakuridhia jambo hilo. Nilisikia Sarah alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine kabla ya harusi yao. Familia ya Kimaro kamwe haina mpango wa kufanya harusi nyingine," Jason alisema.
“Hapana! Iwapo Sarah hataolewa na Alvin, kuna uwezekano mkubwa ataangukia kwa Rodney. Kijana huyo mjinga humlinda Sarah kila wakati. Inabidi tutafute njia ya kumfanya Sarah aolewe hivi karibuni,” Wendy alisema kwa wasiwasi, “Sitakubali Sarah aolewe na Rodney kamwe.”
Mzee Shangwe na Jason pia walitikisa viichwa. Mwanamke kama Sarah Njau lazima asiingie kwenye familia ya Shangwe.
Muda si mrefu baada ya kutoka nje ya jumba kuu la familia ya Shangwe, Lisa aliutoa mkono wake kwa nguvu kutoka kwa Alvin. Alvin alitazama chini kiganja chake tupu na kumtazama kwa hasira. “Sijala kwa sababu nilikimbilia hapa ili kukuokoa.”
“Kwa hiyo? Kama ulituokoa ni lazima nikuache unishike mkono?” Lisa alimtazama kwa ukali. “Basi usinisaidie wakati ujao. Zaidi, Pamela atakuwa mke wa rafiki yako mzuri.”
Pamela, ambaye alikuwa akitembea nyuma, alitaka kutapika damu.
Lisa akamgeukia Pamela na kumuuliza. "By the way, unajua 10% ya hisa za Shangwe Corporation zina thamani kiasi gani ?"
“Ningejuaje? Sipendezwi na—”
“Angalau dola milioni 40.” Alvin alidakia
Pamela alihesabu kwa vidole vyake. Ilikuwa pesa ambayo asingeweza kuipata hata kama angefanya kazi kwa maisha yake yote, lakini bado aliipuuza. "Sahau. Hata kama utanipa dola milioni100, siko tayari kuwa na mpumbavu kama Rodney Shangwe ambaye anajua tu jinsi ya kumlinda b*tch mwenye nyuso mbili kama Sarah Njau.”
Pamela alimtazama Alvin kimakusudi. “Lisa, sitaki kufuata nyayo zako. Ikiwa Rodney ataniambia nipotee na nisipotee, ninaweza kulazwa katika hospitali ya magonjwa ya akili. Sitakuwa na mtu wa kunisaidia kama wewe.”
Alvin aliguna kwa hasira. Kwa kweli alikuwa na hamu ya kumtupa Pamela kwa familia ya Shangwe sasa. Alikuwa tu amefanya upendeleo kidogo, lakini aliharibu kila kitu.
"Haki? Ndiyo maana lazima uwe mwangalifu unapopata mwanaume,” Lisa alisema kwa kumaanisha. "Hasa wale wanaume ambao hupoteza akili zao wanapokutana na b*tches za nyuso mbili. Inabidi ukae mbali nao.”
Baada ya kutoka nje ya makazi ya Shangwe, Alvin alikemewa sana na wanawake wale wawili. Alijiona kama mtu mwenye akili na mwenye nguvu. Vinginevyo, hangeweza kuongoza KIM International na familia nzima ya KImaro huku akiwa amezungukwa na mbweha, lakini, machoni pa wanawake hao wawili, alikuwa mjinga tu. Ilifanya uso wake mzuri kubadilika.
“BwanaKimaro…” Wakati huo, Hans alisimama mbele ya wale watatu akiwa kwenye sedan. “Umeniita kwa—”
"Mrudishe Pamela." Alvin alimkokota Lisa bila neno hadi kwenye gari lake mwenyewe. Tayari alikuwa amevumilia Pamela kama mtu wa tatu asiyehitajika kwa muda mrefu sana.
"Alvin Kimaro, acha. Ninaishi na Pamela, tunaweza kurudi pamoja." Lisa alirudisha mkono wake kwa nguvu lakini hakuweza kujinasua kutoka kwenye mkono wake. Mwili wake ulibanwa kwenye kiti cha gari na Alvin.
“Hata ukisemaje, nimekuokoa leo, kwa hiyo inabidi uniandalie chakula cha jioni. Nina njaa,” Alvin aliinua uso wake mkali na kusema kwa haki.
Lisa alitazama sura yake iliyodhamiria na alijua kuwa asingeweza kujinasua kutoka kwake, kwa hivyo akafunga mkanda wake bila kupenda. "Unataka kula nini?"
"Naweza kula chochote ninachotaka?" Macho ya Alvin yakaangaza. Kabla Lisa hajajibu, tayari alikanyaga kanyagio.
Njiani, alipiga simu. "Peleka kilo 10 za nyama ya nguruwe kwenye Makazi ya Sayuni."
Kama ilivyotarajiwa…Lisa alihema sana. Hakika Alvin alikuwa Alvin. Ubabe wake haukubadilika kamwe.
Muda si muda, gari lilisimama nje Zion Residence. Hapo ndipo mahali alipohamia Alvin baada ya kujitenga na Sarah na kumuacha mtaa wa Oasis. Nyumba aliyoishi Alvin ilikuwa ni jengo lenye ghorofa sita. Alvin alikaa kwenye ghorofa ya juu.
Walipotoka kwenye lifti, Lisa aONA mifuko minne ya nyama imewekwa mlangoni, mara moja kichwa kilimuuma.
Alvin akaingiza neno la siri kwenye mlango huku Lisa akiona na kugeuka na kumwambia, “Umeipata hiyo? Unaweza kuja wakati wowote hata kama sipo."
Lisa alidhihaki, “Kwanini nije hapa? Ili kukupikia? Mimi si yaya wako, na wewe pia hunilipi.”
“Hilo silo nililomaanisha…” Alvin alikosa la kusema na kujihisi hoi.
“Kumbe ulimaanisha nini? Unataka nije hapa kuoga na kulala nawe?” Lisa alisema bila huruma, "Kwako, hizo ndizo kazi pekee nilizo nazo."
“Sikujua hapo awali. Sitafanya hivyo katika siku zijazo.” Alvin alimtazama kwa macho ya kina.
Lisa angeweza kuteka macho meusi ya mtu huyo na uso mzuri hata akiwa amefumba macho. Aliposikiza sauti yake ya chini na yenye sumaku, moyo wake ulikuwa ukirukaruka kama maharage yanayotokota jikoni.
Alvin akafungua mlango, Lisa akaingia. Iliweza kuonekana kwamba Alvin alikuwa amehamia hapo muda si mrefu. Nyumba nzima ilionekana ukiwa, na ilikuwa wazi kuwa mahali hapo hakuishi mtu kabla. Hakukuwa na dalili zilizonyesha kuwa jiko lilitumiwa hapo awali.
"Ulihamia mahali hapa kwa siri ili uweze kuingiza wanawake kwa kumzunguka Sarah?" Lisa hakuweza kujizuia kumdhihaki.
“Nilihamia hapa siku chache zilizopita. Sitarudi kwenye jumba la Oasis tena. Nilifikiria kwenda kuishi kwenye jumba la baharini huko Mombasa nikaona ni mbali,” Alvin alieleza kwa subira, “Nataka kula nyama ya nguruwe choma kama ulizomtengenezea Suzie mara ya mwisho.” Alipokuwa akiongea, alileta mifuko minne ya nyama ya nguruwe.
Uso wa Lisa ulitetemeka. "Usinaimbie unataka nitengeneze nyama zote hizi usiku wa leo?" Ikiwa ndivyo, bila shaka angegeuka na kuondoka mara moja.
Alvin alitazama chini kwa sekunde kadhaa na kutoa mfuko wenye kama kilo nne hivi za nyama. “Pika tu hizi.”
Lisa alipigwa butwaa. Jamani! Kuanzia mwanzo hadi mwisho, Alvin alimchukulia tu kama mpishi. Je, alipendana vipi na mwanamume kama yeye hapo awali? Sahau. Angeweza kuvumilia kwa ajili ya mpango wake. Alifumba macho na kuvaa aproni kabla ya kwenda jikoni kupika.
Alvin alikaa sebuleni akitazama TV. Alitazama nyuma mara kwa mara na kuona mtu mwenye shughuli nyingi jikoni. Moyo wake ulihisi joto.
Hapo awali alipokuwa peke yake hapo, alihisi kwamba mahali hapo palikuwa patupu na kwamba kuna kitu kilikosekana. Sasa, akagundua kwamba palikuwa pamekosa mwanamke. Hakuwa na uzoefu wa aina hii ya hisia hata wakati anaishi katika mtaa wa Oasisi. Ingawa Sarah na Aunty Zara walikuwa pale, hakuwahi kuhisi hivi hapo awali.
Lisa alitumia saa moja na nusu kabla ya kumaliza kuandaa nyama. Alikuwa amechoka kiasi kwamba mikono yake ilishika ganzi na tumbo lilikuwa likiunguruma.
Alvin alitazama vyombo vilivyowekwa pale mezani. Kulikuwa na nyama ya nguruwe iliyochomwa, na nyama ya nguruwe rosti, pamoja na nyama ya nguruwe ya kukaanga. Ndizi zilizochomwa na nyingine za ku-rosti, pamoja na kachumbali.
Alvin alikula kwa kuridhika kwelikweli. Baada ya kula, aliweka iliyobaki kwenye jokofu. Alipogeuka, akamuona Lisa akiwa amekaa akichezea simu yake. Vyombo vilivyokuwa mezani vilikuwa havijaondolewa hata kidogo.
“Vyombo vioshwe…” Aligonga meza na kumkumbusha kwa sauti ya chini.
Lisa aliinua macho kutoka kwenye mchezo wake na kumtazama kwa macho ya makali.
Alvin alieleza, "Hakuna yaya hapa nyumbani, kwa hivyo hakuna mtu wa kufanya mambo haya."
Lisa alicheka. Historia ilikuwa inajirudia. Alizidi kuhisi kwamba tangu zamani alikuwa mjinga kwa kumpenda. “Alvin Kimaro, kuna faida gani mtu kama wewe kutaka mwanamke? Unapaswa kukaa peke yako maisha yote." Lisa aliinuka moja kwa moja na kuondoka zake. Kumtazama tu kulimtia hasira.
Sura ya: 408
Alvin alipomuona Lisa akifungua mlango na kutaka kuondoka, akasogea na kumshika mkono. “Ikiwa hutaki kuosha vyombo, basi usioshe. Sema tu - "
"Alvin Kimaro, inatosha. Ulituokoa kutoka kwa familia ya Shangwe usiku wa leo, kwa hiyo nilipika kwa saa mbili na kukulipa kwa fadhila. Isitoshe, nilikuokoa pia jana. Ni kosa langu kuwa mpole.” Lisa alidhihaki, “Usinitafute siku za usoni. Sitaki kukupikia kwa uchungu na kuishia kuwajibika kuosha vyombo na kusafisha baada ya kukupikia pia. Ninapendekeza upige simu namba hii ikiwa unahitaji kitu katika siku zijazo. ” Lisa akatoa simu yake na kuvuta mawasiliano ili amuoneshe.
Alvin aONA kuwa namba hiyo imehifadhiwa kama 'Wakala wa Utunzaji wa Nyumba'. Uso wake mzuri ukasinyaa ghafla.
Lisa alikumbusha kwa dhati, “Usifikiri kwamba watunza nyumba ni wanawake wakubwa. Kuna wengine ambao ni vijana na hawajaolewa. Unaweza kuchagua yoyote kati yao ukiona anafaa kwako.” Kisha akaufunga mlango na kuondoka zake. Ilikuwa ni kana kwamba ilikuwa inamkera sana kumtazama.
Kifua cha Alvin kilimpanda kwa hasira. Wakati anamfuata, sura yake ilikuwa imetoweka. Aliporudi ndani na kuona meza imejaa vyombo vilivyotumika. Alihisi huzuni.
Alikuwa ametoka tu kumtaka aoshe vyombo. Je, kulikuwa na haja ya kuongea mambo mengi hivyo? Ikiwa hakutaka kuosha, basi angesema hivyo tu. Haikuwa kama alikuwa akimlazimisha aoshe vyombo.
Alichukua simu yake na bila fahamu alitaka kumpigia Chester kwa ushauri, lakini mara akaacha. Chester na Sarah pia walikuwa marafiki. Ikiwa Chester angegundua kuwa Alvin alikuwa na Lisa, bila shaka angeanza kumsumbua tena.
Alifikiria jambo hilo na kuingia mtandaoni kwa jina tofauti ili kuficha utambulisho wake, na kuuliza: [Nilimwalika msichana ninayempenda kupika nyumbani, lakini nilipomwomba aoshe vyombo, alikasirika na kuondoka. Je, ni kosa langu au mwanamke huyo ana akili finyu sana?]
Chini ya nusu saa baada ya kuichapisha, sehemu ya maoni ililipuka.
[Oh Mungu wangu, siwezi kuamini kwamba kuna mtu aliuliza swali kama hili. Mwanamke huyo atakuwa na bahati mbaya kiasi gani kupendwa na mwanamume kama huyu?]
[Una ujasiri mwingi wa kuuliza ikiwa mwanamke huyo ana mawazo finyu! Wewe umeyapima mawazo yako na kyaona ni finyu kiasi gani?]
[Rafiki, kama mwanamume, ninakuambia hili kwa fadhili kwa ujasiri: Hutaweza kupata rafiki wa kike kama huyu.]
[Nadhani hupaswi kupata rafiki wa kike. Pata tu mfanyakazi wa nyumbani.]
[Kama ningekuwa mwanamke huyo, si tu ningekimbia, ningekublock pia.]
Alvin alikasirika sana alihisi kana kwamba anakaribia kulipuka. Wanamtandao hawa walikuwa wamerukwa na akili. Walimaanisha nini kusema alikuwa na mawazo finyu? Walimaanisha nini kusema asingeweza kupata rafiki wa kike? Siku zote alikuwa akifuatiliwa na kila aina ya wanawake.
Alikasirika na kufuta chapisho hilo. Alijilaumu kwa kuuliza swali lisilo na maana kama hilo mtandaoni.
Baada ya kufuta chapisho hilo aliitafuta namba ya Lisa na kumpigia. Hata hivyo, kilichomjibu ni sauti ya kike ya kiotomatiki ikisema, "Namba ambayo umepiga haipatikani kwa sasa." Kisha akajaribu tena dakika moja baadaye lakini akapata jibu lile lile. Dakika tano baadaye, bado ilikuwa vile vile.
Nusu saa baadaye, alikuwa na uhakika kwamba kweli alikuwa amechezea block. F*ck.
•••
Baada ya Lisa kurudi nyumbani kwake, Karen Estate, Pamela, ambaye alikuwa ametoka kuoga, mara moja alikimbia na kumkonyeza macho. "Hebu niangalie kama nguo zako ziko sawa. Halo, nguo zako zimekunjamana na nywele zako zimetibuka sana. Unaonekana umechoka pia. Je, nyinyi wawili…” Pamela alitabasamu kiutata.
Lisa alifuta macho yake yenye usingizi. “Ondoa mawazo hayo machafu. Nilikwenda kwake na kumpikia kwa saa mbili. Nina mikwaruzo kwenye mikono yangu kutokana na kukata nyama nyingi sana.”
Pamela kimya aliitazama mikono yake yenye rangi nyekundu na akakosa la kusema.
Lisa alionekana kama anataka kulia na akalalamika, "Kilo 10 za nyama. Nilizikatakata kwa muda mwingi kabla ya kumwekea kwenye friji. Kisha, nilimpikia nyama ya nguruwe iliyochomwa, rosti, nyama ya nguruwe kukaanga, ndizi, kachumbari… Nilikuwa nimemaliza kula akaniuliza kwanini siendi kuosha vyombo. Mimi…?!” Alikunywa glasi kubwa ya maji kwa hasira. "Hivi, unaweza kuamini kwamba sikunywa hata glasi ya maji nyumbani kwke?"
Pamela akampiga bega kwa huruma. "Ulikuwa kipofu kiasi gani kumpenda hapo awali?"
“Unajua kwamba mimi pia ni kipofu?” Lisa alitazama juu na kuhema. “Niliblock namba yake mara tu nilipotoka. Inatia hasira kiasi gani.”
"Umefanya vizuri. Lazima uwe umechoka. Nenda kaoge kisha ulale.” Pamela alimfariji. "Ninaamini kwamba baada ya tukio hili, moyo wako utakuwa mtulivu na hatakusumbua tena."
•••
Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili, Alvin alipotoka kwenye lifti kuingia ofisini kwake, alimsikia Hans akiongea na wanawake kadhaa katika idara ya katibu kwenye korido.
"Hans, niONA mwanamume mcheshi sana kwenye group la facebook jana akiuliza swali mtandaoni jana. Mwanamume huyo aliuliza, 'Nilimwalika msichana ninayependa kupika nyumbani, lakini nilipomwomba aoshe vyombo, alikasirika na kuondoka. Je, ni kosa langu au mwanamke huyo ana mawazo finyu sana?' Mungu wangu, kweli dunia ni kubwa. Kuna kila aina ya wanaume wa ajabu huko nje."
Hans alicheka. “Huyo mtu ana kichaa. Alimwalika mwanamke nyumbani pake, akamwomba ampikie, akampikia, kisha akamtaka aoshe vyombo pia? Msumbufu wa namna hii atakimbiwa na wanawake wote.”
"Haki? Hata alikuwa na ujasiri wa kuuliza swali mtandaoni! Inatosha kuwa hajitambui, lakini alikuwa na jeuri ya kumtuhumu mwanamke huyo kuwa na mawazo finyu sana.”
"Kuna wanaume wa ajabu zaidi siku hizi. Ni bora kukaa mbali na watu kama hao ikiwa utakutana nao."
Wakati fulani, kila mtu ghafla alihisi baridi ikitoka nyuma yao. Ilikuwa karibu kiangazi, lakini waONA kana kwamba kulikuwa na baridi zaidi kuliko majira ya baridi.
Mtu mmoja aliita, "Bwana Kimaro." Walipotazama nyuma, waONA sura nzuri ya Alvin lakini yenye huzuni.
“Bwana Mkubwa…” Hans alieleza kwa woga, “Saa za kazi hazijaanza, kwa hivyo sisi…”
"Hans. ” Alvin alimwangalia kwa macho ya kifo. “Ingia ndani.”
Kisha, Alvin akaingia ofisini.
Hans alimfuata kwa hofu na kufunga mlango. “Bwana Kimaro, samahani. Sitawahi kuzungumza tena na wengine kwenye korido…”
“Hans, mtu mwendawazimu mliyekuwa mkimjadili hapo awali ni mimi.” Alvin akavua koti lake na kulitupia kwenye kiti chake cha ngozi. Macho yake yalikuwa ya huzuni. “Mimi ndiye niliyeuliza swali hilo mtandaoni. Mwanamume yule yule uliyesema hatapata rafiki wa kike maishani mwake.”
Hans alishtuka. Alikuwa na hamu ya kujiua papo hapo. Ni maneno gani ya kuudhi aliyoyasema hapo awali? Hakuweza kukumbuka hata kidogo.
“Bwana Mkubwa, samahani. Sikujua, ” Hans aligugumia, “Ni… nilifikiri ni mhuni tu na mtu asiyejitambua wa kawaida. Bila shaka… kwa mwanamume mtanashati, tajiri, na mashuhuri kama wewe, kuna wanawake wengi walio tayari kukupikia na kukuoshea vyombo. Haiwezekani kwako kukosa rafiki wa kike.”
Alvin alikoroma kwa hasira. "Hivyo sivyo nilivyokusikia ukisema."
Moyo wa Hans uliruka hadi kifuani mwake. Hakutaka kitu zaidi ya kutoweka. Hakuweza kuelewa. Si yeye peke yake aliyekuwa akipiga porojo. Mbona bosi alikuwa anamsumbua yeye tu?
"Basi nijibu swali hili." Alvin aligonga meza na kusema kwa sauti kubwa, “Lisa… Kwanini alikasirika na kuondoka? Je, kweli nilifanya kitu kibaya? Nifanye nini sasa?”
"Bwana Mkubwa, kwa heshima zote, kwa sasa ... kwanini usimchumbie tu kama bado unampenda?" Hans aliuliza kwa makini.
Alvin alimdhihaki na kumtazama. “Ni lazima nimchumbie? Unapaswa kumjua Lisa vizuri kuliko mtu yeyote. Amenipenda kwa muda mrefu, lakini nilimuumiza siku za nyuma na kumfanya akose raha. Hata hivyo, ninajishusha kwa ajili yake.”....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
