JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................321-322

Sura ya 321

Baada ya Amba kuwapigia simu wahahisa kadhaa wa Mawenzi, alimgeukia Lisa akiwa amekasirika kwa huzuni. “Mwenyekiti Jones, wakurugenzi wa Mawenzi Investments hata hawakupokea simu zangu. Wapo waliojibu lakini walikata simu kabla sijamaliza kuongea. Ninasikitika kusema kuwa Chris Maganga ndiye pekee atakayehudhuria mkutano huo.”
"Mjomba Chris bado ni yule yule, sivyo?" Lisa alicheka huku akimwagilia maua kwenye kibaraza.
"Haujakasirishwa na hilo, Mwenyekiti Jones?"
“Usijali. Mkutano mkuu utaendelea kama kawaida. Unaweza kwenda nyumbani sasa. Kuna mgeni atatembelea nyumbani kwangu baada ya muda mfupi.” Lisa alimkonyeza kwa namna ya kinyonge.
Kwa mtazamo wa Lisa wa kujiamini, Amba aliondoka kwa mashaka.
Muda mfupi baada ya Amba kuondoka, Lisa alipiga simu ya video ili kuzungumza na watoto wake wawili nchini Marekani.
“Nimekukumbuka, Mama.” Suzie alionyesha sura yenye machozi kwenye uso wake mzuri wa mviringo. Hata hivyo, Lisa alipandwa na hasira mara tu alipoona chokoleti mdomoni mwa Suzie.
“Susan Jones, ulimshawishi ma’mdogo akununulie chokoleti tena, sivyo?” Suzie akapepesa macho yake yasiyo na hatia. “Hapana, Mama. Unanisingizia!”
“Huna akili Suzie.” Lucas alimtizama dada yake na kusema. “Ona. Hukusafisha chokoleti pembeni mwa mdomo wako.”
Kwa mshtuko, Suzie alilamba chokoleti kwenye ukingo wa mdomo wake haraka. Muda si muda alikuwa msafi na kusema bila hatia, “Sikula. Godmother alikula chokoleti na kunibusu baadaye.”
Lisa alijipapasa paji la uso wake, akacheka huku akishangaa kwanini amezaa na mtoto wa aina hiyo ambaye alikuwa mjuzi wa kusema uongo.
Lucas alisema, “Unafikiri Mama atakuamini tena, mjinga wewe!”
“Nani mjinga sasa? Sichezi na wewe tena.” Suzie alikoroma. Aligeuka na kumpuuza Lucas.
Lucas alishusha pumzi na kumuuliza, “Mama unaendeleaje huko? Baba alikuletea shida? Unaweza kupambana na kila kitu? Unahitaji nije nikusaidie?”
Lisa alishindwa cha kusema. Mtoto wake alikuwa na maswali kama polisi.
Wakati huu, mtu alikuwa akipiga hodi mlango kwa teke.
“Mpenzi, nina jambo la kufanya sasa. Tutaendelea usiku wa leo. Muah!”
Lisa akakata simu. Alipokaribia tu mlangoni, mlango ulipigwa teke kwa nguvu. Alvin aliingia ndani huku uso wake ukiwa na huzuni, macho yake yakionyesha ukali.
“Lisa unathubutu vipi kumsababishia Sarah matatizo?! Unabipu kifo, huh?" Alvin alinyoosha mkono wake mkubwa kuibana shingo yake bila kusita.
Lakini, Lisa alikuwa tofauti na hapo awali. Alimpanchi kwa uangalifu kabla hajamfanyia chochote.
Alipogundua umachachari wake, Alvin alitania, "Inaonekana kama Maya yuko sahihi. Umepata ujuzi fulani kwa miaka hii michache, lakini uwezo wako si lolote kwangu.”
"Siku zote nimekuwa nikifahamu ujuzi huu na hakuna ubaya kuuweka katika vitendo kwa ajili ya kujilinda sasa hivi." Lisa aliinua uso wake mzuri wa umbo la mviringo. Alipepesa macho yake mazuri na kutabasamu kwa busara. “Hubby, umekuwa si mwaminifu baada ya kuachana na mimi kwa miaka michache. Una mawazo ya kumuua mkeo mchana kweupe, huh?"
“Uliniita nani?” Uso mzuri wa Alvin ulikaribia kubadilika. “Nani anakupa haki ya kuniita hivyo? unaota?.”
“Nasema ukweli tu. Tazama, hiki ndicho cheti chetu cha ndoa.” Lisa akakitoa na kukizungusha.
“Una wazimu, Lisa? Kwanini unanionyesha vitu vya aina hii?” Alvin alimkaripia vikali.
Tabasamu gumu lilienea kwenye uso wa Lisa. Maneno hayo yaligonga kengele kwenye kichwa chake. Hapo awali Alvin alikuwa amezoea kumtishia kwa cheti cha ndoa kila alipotaka kudai talaka. Kwa bahati mbaya, kila kitu kilikuwa kimebadilika tangu wakati huo.
"Wewe si mke wangu." Alvin alimkubusha.
Lisa alicheka ghafla. “Alvin, ingawa ndoa yetu ilikuwa ni makubaliano tu, lakini nilishawahi kukuomba hata senti? Mawenzi Investments ndicho kitu pekee ambacho mama yangu aliniachia na ndicho kitu muhimu zaidi kwangu, hata hivyo ulimpa Sarah. Unaongeza mafuta kwenye moto. Ikiwa ulitaka kumpa kitu, ulipaswa kumpa kitu ambacho kilikuwa chako wakati huo. Kwanini umpe kilicho changu?”

Kadiri Lisa alivyozidi kuongea, ndivyo alivyokasirika zaidi. Licha ya kujifunza kudhibiti hisia zake kwa miaka hii michache, bado hakuweza kujizuia lakini kupoteza utulivu wake wakati huo.
Alvin ambaye tayari alikuwa amefura kwa hasira, alishindwa kujibu swali lake. "Ningejuaje kuwa kampuni hiyo ndiyo urithi ulioachiwa na mama yako?"
Lisa alitabasamu. "Ni kweli. Hukujua kuhusu hilo. Hujui lolote.”
Alijua kweli. Ni kwamba tu alikuwa amesahau kutokana na kuharibiwa kumbukumbu muhimu. Hata hivyo, asingemsamehe kwa sababu tu alikuwa amesahau.
“Ni sawa ikiwa umeisahau, lakini huwezi kuchukua kilicho changu na kumpa mwanamke wako.” Lisa alifoka.
“Hata hivyo, hukupaswa kumshambulia Sarah,” Alvin alisema kwa uchungu, “Ni kosa lako kwamba ulighushi kifo chako. Sarah alijitahidi sana kuisimamia Mawenzi Investments na ameboresha utendaji wa kampuni kwa kiasi kikubwa.”
"Kwani hakuna watu wengine katika Mawenzi Investments? Hapo awali, Meneja Mkuu Ngololo alifanya kazi nzuri katika kusimamia kampuni. Kwanini mlimshusha cheo?” Lisa alichukizwa sana. “Sarah alisomea saikolojia na sio usimamizi wa biashara. Ikiwa anataka kusimamia kampuni, anaweza kusimamia New Era Advertisings, hiyo ndiyo inayomhusu. Kwanini anang’ang’ana na Mawenzi Investments?"
Lisa alitabasamu ghafla bila furaha na kujibu, “Anataka tu kuninyang’anya vitu vyangu vyote, sivyo? Anaweza pia kunyakua Ngosha Corporation ya baba yangu pia?”
“Inatosha. Sarah si mtu wa aina hiyo.” Alvin alishindwa kujizuia kumkatisha. "Mwanzoni, alipendezwa na biashara ya uwekezaji. Sikuwa na kampuni zozote za uwekezaji, hivyo nilimwacha amchukue Mawenzi Investments.”
“Naam, basi niwashukuru ninyi wawili kwa kuisimamia vizuri Mawenzi Investments kwa niaba yangu.” Lisa alikunja midomo yake bila kutarajia. “Nimpe thawabu gani kwa ajili ya kazi yake ngumu?”
“Lisa, nimekerwa sana na utani wako. Unachukiza.” Macho ya Alvin yalidhihirisha chuki yake kwake.
“Sawa. Ikiwa hutaki kuona upande wangu wa kuchukiza, ni bora uirudishe Mawenzi Investments kwangu haraka iwezekanavyo na kumfukuza Sarah. Nitarudi kwenye kampuni na kupanga upya kila kitu kesho.” Lisa hakuwa na wasiwasi kabisa juu ya jinsi alivyokuwa akimchukulia.
Alvin alijawa na hasira. Lisa alimfanya aonekane kama alikuwa na hamu ya kumiliki kampuni yake. "Sina haja kabisa kampuni mbaya kama Mawenzi Investments. Baada ya kusema hivyo, ni lazima umuombe msamaha Sarah hadharani kesho.”

Lisa alichimba masikio yake kwa kidole na kusema. “Unataka nimuombe msamaha? Endelea kuota."
"Sitakurudishia kampuni hiyo." Alvin alitoa kicheko jeuri. "Wanahisa wa Mawenzi Investments ni wajanja. Hata ukiitisha mkutano hawatakujali kwa sababu wanapokea maagizo yangu.”
“Sawa basi.” Lisa hakuwa na wasiwasi hata kidogo. Alipeperusha cheti cha ndoa na kuongeza, “Katika hali hii, nitapiga picha na kuposti cheti hiki mtandaoni. Nitadai kwamba bado tumeoana. Miaka mitatu iliyopita, ilibidi niuambie umma kwamba tuliachana kwa sababu ulinitishia na baba. Unadhani watu wataacha kumshambulia Sarah baada ya kipande hiki cha habari kufichuliwa? Nadhani hakuna mtu ambaye amezungumza kuhusu uhusiano wenu katika miaka michache iliyopita.”
“Usithubutu,” kauli ya Alvin ikabadilika huku akimwonya kwa uchungu.

"Bila shaka, sitaogopa hata kidogo kufanya hivyo." Lisa aliinua kichwa chake huku akifichua uso wa dharau.

Alvin alimtupia jicho na kukamata cheti cha ndoa ghafla. Mara Lisa akageuka na kuking’angania.
Kifua cha Alvin kilimgonga Lisa mgongoni. Huku nywele zake ndefu zikining’inia chini, aliweza kunusa kwa urahisi harufu hafifu ya kama ya maua alipoinamisha kichwa chake. Hakuweza kukumbuka ilikuwa harufu ya maua gani, lakini lilikuwa na harufu nzuri sana. Sio tu kwamba alipendezwa na harufu, lakini pia alitulizwa nayo na kuliwazwa kabisa. Alinukia vizuri zaidi kuliko Sarah.

Alvin alipokuwa akitoka nje kwa muda, Lisa alimsukuma na kukimbilia chumbani kwake mara moja. Akiogopa kwamba angekimbia, bila fahamu alimvuta mkono wake laini na mwembamba kumwelekea. Kutokana na nguvu nyingi za Alvin, aliishia kujigonga mikononi mwake. Kwa wakati huu, mgongo wake ulikuwa umekwama kwenye kifua chake. Huku akiuma meno alitumia mkono mmoja kumshika Lisa na mwingine kujaribu kumpokonya cheti cha ndoa mkononi.

Sura ya: 322

Lisa alijitahidi kujinasua kutoka kwa Alvin bila kutambua kwamba alikuwa akizunguka katika mikono yake. Akiwa amegundua mabadiliko ndani yake, uso wake ulikuwa tayari umejawa na aibu. "Alvin, wewe ni mtu wa ajabu sana."

Alvin naye alionekana kuwa na aibu na mshtuko sana. Siku zote alikuwa akidhani kwamba asingesisimka tena kwa mwanamke kwa sababu kila alipokutana na Sarah, bila fahamu alihisi kuchukizwa naye. Hata alishuku kuwa hakuwa na uwezo tena wa kumridhisha. Hakutarajia kwamba angesisimka tu kwa kumkumbatia Lisa. Hisia hii ilimfanya adhalilike hasa, na kwa namna fulani alipoteza udhibiti pia.

Akiwa amekasirishwa na matamshi ya Lisa, alisema, “Ni nini kinanifanya niwe mtu wa ajabu? Wewe ndiye wa ajabu. Mimi ni mwanaume wa kawaida.”

“Kwanini ulitembelea kitengo cha andrology hospitalini asubuhi ya leo,” Lisa alifoka.

Alvin aliona aibu hata uso wake ukatepeta ghafla. Kama angekuwa na uwezo angeyeyuka tu na kupotelea hewani. "Nimekuambia kwamba nilienda huko kumsindikiza Hans."

“Unanichukulia kama mjinga? Kwanini bosi amsindikize mfanyakazi wake huko?” Lisa alimsukumia mbali. Alimuonyesha mlango wa kutokea na kusema kwa hasira, "Toka nje."

Alvin aliutazama uso wake uliokuwa umekunjamana mithili ya waridi zuri lililokaribia kuchanua. Alihisi usumbufu fulani. “Kwanini nitoke?”

"Hakuna uhusiano wowote kati yangu na wewe." Lisa alijitahidi kumkumbusha ukweli ambao hata hivyo Alvin hakuwa tayari kuukubali.

“Nina uhakika bado nina uhusiano na wewe. Bado una cheti cha ndoa yetu kwa hivyo kishria wewe bado ni mke wangu.” Alvin alifoka ghafla na kumsogelea taratibu.

Lisa alishangazwa na tabia yake ya kukosa aibu. “Alvin, kwanini unakosa adabu? Umekiri kuwa mwaminifu kwa Sara. Hata kama hutaki kuniheshimu mimi, kwanini hutaki kumheshimu Sarah basi?”

Jina 'Sarah' lilionekana kama ndoo ya maji baridi iliyomwagiwa juu yake. Alikunja uso kwa hatia na kukodoa macho ghafla. Ni lazima alirogwa atoe maneno ya kipuuzi kama yale. “Nilikuwa nakukebehi tu. Sura yako tu kwanza inanichukiza sana”

Kwa hayo, Alvin alikoroma na kuelekea bafuni. Lisa alitoa kicheko cha dharau. Alidai kuwa sura yake ilimchukiza kwanini sasa anatumia bafu lake? Huenda mwanamume huyu alitaka kwenda kujidhuru tena bafuni mwake ili kupunguza hasira. Ugonjwa wake ulionekana kuwa haujamwisha.

Baada ya kusubiri na kuona kimya kwa dakika kama kumi hivi, Lisa aliamua kwenda kuchungulia. Alvin alikuwa bado yupo ndani.
Kwa hali aliyomkuta nayo, alihitaji kweli hata kutembelea kitengo cha andrology? Alvin alikuwa anajaribu kupoza msisimko wake wa mapenzi kwa kujichua, na mtambo ulikuwa umesimama vizuri tu. Sasa kwanini kulikuwa na tatizo la unyumba kwenye uhusiano wake na Sarah? Alikuwa akikwama wapi, au ni kwa sababu Sara alikuwa mgumu kuridhika? Lisa alitoa mshtuko.

Wakati huo, Lisa alihisi njaa ghafla. Hakuwa amekula chakula cha mchana, kwa hiyo alielekea jikoni kupika makaroni, akaweka na jibini, kisha akaongeza na soseji. Dakika ambayo Alvin alitoka bafuni kwa unyonge, harufu ya makaroni na jibini na soseji ikitoka jikoni mara moja ikajaza pua yake. Harufu ya ajabu mara moja ilimfanya awe na njaa.

Alitembea hadi jikoni na kumwona Lisa ambaye alikuwa amevaa kitop tu chepesi sana na kipensi kifupi sana, akiwa anakata soseji. Alionekana kupendeza huku nywele zake zikibembea kama mkia wa farasi. Hisia ambazo alikuwa ametoka kuzituliza bafuni zilibubujika tena ndani yake.

Alvin aliuma meno yake na kwenda kwa Lisa. Kisha, akasema bila chuki, “Unajaribu kunitega?”

“Huh?” Lisa alishikwa na mshangao kabisa. Macho yake meusi ya kupendeza yalifichua hali ya kutokuwa na wasiwasi na kujiamini. Hakutambua jinsi alivyoonekana kuwa mwenye kuvutia wakati huo. "Nikutege kwa lipi?"

"Unanifahamu vizuri kuliko mtu mwingine yeyote." Alvin alikazia macho yake kwenye uso mzuri wa Lisa na kumdhihaki kabisa. Alitamani hata ayashike matiti yake yaliyotuna na kukinyanyua kile kitop chepesi kifuani kwake. Midomo yake nayo ilikuwa kama inamualika kwa busu zito.

Lisa alitazama chini bila kumjali. “Hatimaye umemaliza kumwaga wazungu wako bafuni kwangu, huh?”

Alvin alimtazama kwa ukali, uso wake ukawa mbaya bila yeye kujitambua. “Lisa Jones, una mawazo gani? Huna aibu?”

Lisa aliinua macho yake. Kimsingi hakuwa akimpenda, lakini kwanini alikuwa akipandsha hisia baada ya kumuona? Alikuwa akijaribu kupoteza uvumilivu wake kidogokidogo? “Nilikuwa nawaza tu kwamba kwa hali hiyo, huna haja ya kutembelea kitengo cha andrology! Sarah ndiye anapaswa kumuona daktari. Kama mwanamke, hakuna haja ya kutamani sana. Kwa hali yako, anapaswa kuridhika.”

“Sarah hafanani na wewe,” Alvin alimdhihaki kwa hasira licha ya kuufahamu ujumbe wake.

Lisa hakuwa na neno. Alvin alikuwa ameishi naye kwa muda kabla hajaondoka na hata akapata watoto pamoja. Aliijua hamu yake na uwezo wake. Wote wawili hawakuwa wamezowea mbio za marathoni kitandani. Huenda Sarah alikuwa ni mtu aliyependa kuzama kina kirefu kwenye bahari ya mahaba kabla hajaibuka nchi kavu na Alvin hakuwa na uzoefu huo. Lisa alianza kutilia shaka hilo lakini hakuwa tayari kulijadili akilini mwake, akabadili mada.


“Umeamuaje?” Lisa aliuliza ghafla.

Alvin alipigwa na butwaa kwa muda, huku uso wake ukiwa umekunjamana. "Unazungumza juu ya Mawenzi?"

"Ni juu yako ikiwa utanirudishia, lakini haiwezekani kwangu kuomba msamaha kwa Sarah," Lisa alisema bila kujali, "Baada ya kusema hivyo, uvumilivu wangu una mipaka yake. Unapaswa kuamua kesho. Vinginevyo, ninaogopa sitaweza kudhibiti mikono yangu na kuishia kufichua maovu mliyoyafanya.”

“Lisa Jones, unafahamu hata mipaka yako? Unathubutuje kunitisha?!” Alvin alipandwa na hasira, macho yake yakiwa yamejawa na huzuni.

“Kwanini? Unapanga kuniua, huh?” Lisa hakuwa na woga.

Uso mzuri wa Alvin ukaingia hasira. Machoni mwake, je, alikuwa kichaa tu aliyeua watu kinyama? “Unafikiri sitaweza kufanya hivyo?” alimuonya vikali.

“Najua unaweza kufanya hivyo. Hakika sitatilia shaka, lakini huwezi kuninyonga kwa urahisi sasa.” Lisa alitabasamu. "Labda mimi si mkubwa kama wewe, lakini tukianza kushambuliana, itawatahadharisha majirani na mtaa mzima. Zaidi ya hayo, tangu ulipoingia katika mtaa huu, mienendo yako yote imerekodiwa kwenye kamera za uchunguzi. Nikifa, hakika hutaweza kuondoka salama. Mwenyekiti Kimaro, hata kama unapanga kuficha ukweli kupitia hongo, tukio hili bila shaka litapiga kengele. Kwa mfano, familia ya Campos, ambayo imekuwa ikipanga njama na kugombea kuwa Mtanzania mahiri zaidi nchini Kenya, pengine itachukua fursa hiyo kuharibu sifa yako na hata… kukuweka kuzimu.”

"Ni uchambuzi gani wa kina umetoa." Alvin alikasirika sana. Ina maana alikuwa na mawazo kwamba angemuua? Ingawa hakuwahi kufikiria kufanya jambo lolote lisilo halali, nia yake ilikuwa nini kumkasirisha?

"Asante." Lisa aliinamisha kichwa chake na kuendelea kukata soseji. "Hapo awali, uliweza kunitisha na baba yangu na Pamela. Lakini sasa kwa kuwa baba yangu amepata nafuu na Pamela hayupo, niko peke yangu. Sina cha kupoteza.”

Alvin alimkazia macho mgongoni. Hakuwa na udanganyifu kwamba maneno yake yalikuwa ya kweli. Hakika, hakuna kitu tena ambacho angeweza kutumia kumtishia mwanamke huyu.

Walikaa kimya kwa nusu dakika kabla ya Alvin kusema, "Ninaweza kuahidi kuirudisha Mawenzi kwako, lakini lazima tupeane talaka."

"Hapana." Lisa alimkataa kabisa bila kuinua kichwa chake.

Alvin alilipuka kwa hasira. “Kuwa na shukrani, tayari nimeshafanya makubaliano.”

Lisa aligeuza kichwa chake na kuinua macho yake. "Kama usingemteua Sarah kama Mwenyekiti wa Mawenzi, ningekubali talaka. Lakini ulinikasirisha, haswa leo nilipojua kuwa ulimfanya Cindy kuwa balozi wa Mawenzi. Una maana gani kukusanya watu hao ninaowachukia na kuwaweka kwenye kampuni yangu? Kwanini usimwombe Lina ajiunge pia? Kwa kuwakusanya hao wanafiki watatu, unaweza kutimiza matakwa yako yote.”

Akiwa ameudhishwa na shutuma zake, Alvin alidhihaki, “Kwa hiyo sasa unamchukia kila mtu niliyemteua? Ulikuwa umekufa, unategemea kampuni ingeongozwa na nani?".......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.