JINA LA SIMULIZI............................LISAAUTHOR...........................JOMBA WAJO SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY WHATSAPP...........................0628924768 SEHEMU YA........................173 -174-175
Sura ya:173
Lisa na Kelvin walipokuwa wakielekea upande huo, Alvin alimtazama Kelvin kwa hasira.
"Wewe ni…?" Alvin aliuliza kwa kejeli utadhani hamfahamu kabisa.
“Yeye ni mchumba wa Lisa kutoka Golden Corporation.” Joel Ngosha aliwahi kutoa utambulisho haraka haraka.
"Sijawahi kumsikia." Alvin alitazama pembeni na kuongeza maneno ya kejeli kwa sauti ya dharau. “Kwa hiyo, mtu yeyote anaruhusiwa kuketi kwenye meza ya heshima ya familia ya Ngosha, sivyo?”
Kwa hayo, uso wa kifahari na mzuri wa Kelvin ulibadilika na kufunikwa na hasira. Lisa alihisi kana kwamba amepigwa kofi usoni. Alibaki katika hali ya aibu huku Melanie alicheka kwa dharau.
“Hasa. Angalia tu Bwana Kimaro ni nani. Sio kila mtu anaweza kukaa naye." Mzee Ngosha alionekana kutofurahishwa pia.
Bibi Ngosha aliona aibu sana kwa sababu yeye ndiye aliyemwomba Lisa aketi pale na Kelvin.
Nitaenda kwenye meza nyingine." Kelvin alimpiga Lisa nyuma ya mkono wake. Kisha, akageuka na kuelekea kwenye meza nyingine ya kawaida.
“Subiri. Tutaenda wote. Hata hivyo mimi ni mtoto wa nje, sistahili kuketi na Bwana Kimaro pia.” Lisa alimfuata Kelvin. Wote wawili hatimaye waliketi kwenye meza nyingine ndogo tu ya kawaida.
Alvin aliuma mdomo wake na kulazimisha tabasamu la kuridhika huku akijiachia kwenye kiti cha heshima.
Mzee Ngosha aliibuka na kumbembeleza Alvin. “Pole sana, Bwana Kimaro. Huo ulikuwa utoto tu wa Lisa. Usizame kwenye kiwango chake. Yeye ni binti haramu ambaye alitoka kijijini, kwa hiyo hana ustaarabu kabisa.” Baada ya hapo, alijifanya kutabasamu.
“Baba…” Uso wa Joel ulijawa na aibu. Hakuweza tena kuvumilia.
"Nyamaza." Mzee Ngosha alimkazia macho Joel. Kisha, akatoa ishara kwa Melanie kwa macho yake.
Melanie aliukumbatia mkono wa Alvin mara moja na kuongea kwa kujishaua. "Bwana Kimaro, ninaahidi kwamba hutawaona wawili hao tena utakapotembelea familia ya Ngosha wakati ujao."
"Ndio ndio. Bila kujali ni tukio gani, hawatakaribishwa tena hapa.” Mzee Ngosha alijitahidi sana kumbembeleza Alvin.
Alvin aliuma mdomo wake kidogo, jambo ambalo lilionekana kumaanisha kuridhika. Kwa kweli, wale waliomfahamu walijua kwamba alikuwa akiudhika zaidi moyoni mwake.
Lisa, ambaye alikuwa kwenye meza nyingine, kwa kawaida alisikia mazungumzo kati ya watu hao. Alijua kwamba kila mtu pale mezani alikuwa akimtazama kwa namna ya nderemo bila hata kumuonea huruma. Uso wake uligeuka kwa hasira kidogo kidogo. Kelvin alishikilia mkono wake kwa nguvu chini ya meza. Ilikuwa ni mara ya kwanza kujihisi mnyonge sana. Kwa unyonge aliopata siku hiyo, aliapa kwamba alipaswa kuwa na nguvu ili kuwalipa kwa faida.
Baada ya chakula cha mchana, Lisa alipotoka sebuleni, alikutana na Farres ambaye alikuwa akitoka nje ya choo cha kiume. Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 40 hivi alikuwa amejengeka kwa misuli yenye nguvu na hakuwa amenyoa nywele. Alionekana mbaya na hatari.
Walipokabiliana bila kupishana, Farres alimpa tabasamu baya. "Una ustadi mkubwa wa kuendesha gari, msichana mdogo. Hongera kwa kunusurika kwenye ajali. Siku nyingine hutakuwa na bahati kama hiyo.”
Uso wa Lisa ukaingia giza. Alithubutu vipi kujitapa mbele yake kuhusika na ajali ile?! "Jitape sana lakini mwisho wako haupo mbali." Lisa naye alimtishia.
“Haha. Wakati Melanie anakuwa Madam Kimaro, nitakuua na hakuna mtu atakayesema chochote kuhusu hilo.” Farres aliinua mkono wake na kufanya kitendo cha kukata shingo yake. Kisha, akaangua kicheko kisicho na adabu.
Macho ya Lisa yalidhihirisha mshtuko. Huku akitetemeka, alisema, “Kwa kuzingatia sauti yako ya kiburi, lazima uwe umefanya ukatili mwingi. Kifo cha mama yangu nina uhakika kinahusiana na familia yako.”
Farres alipigwa na butwaa kwa muda. "Mama yako alikufa katika kimbunga huko Kigoma. Ina uhusiano gani na mimi? Sheryl alikuwa na bahati mbaya sana kufa akiwa bado binti mdogo, lakini afadhali uangalie," Farres alimuonya na kisha akaondoka akiwa ameduwaa.
Lisa alimkazia macho katika hali ya kuchanganyikiwa. Ikiwa haikuwa familia ya Mahewa iliyomuua Sheryl, basi nani?
Karamu iliisha. Lisa na Kelvin walipokuwa wakielekea kwenye maegesho ya magari, alipokea ujumbe kutoka kwa Alvin. [Nakungoja nje ya hoteli. Njoo hapa.] Lisa alishindwa tu kulia. Jinsi Alvin alivyokuwa na aibu kumtafuta! Aliufuta ujumbe huo mara moja.
Muda mfupi baadaye, hata hivyo, Alvin alimtumia video ya kucheza kwake akiwa amevalia mavazi ya aibu. Lisa alisaga meno yake. Aligeuka na kumwambia Kelvin, “Nakumbuka tu kwamba ninahitaji kukutana na bibi yangu ili kushughulika na jambo fulani. Si lazima unirudishe nyumbani.”
“Sawa. Nipigie mara tu utakaporudi." Baada ya kumkumbusha, Kelvin alimtazama akiondoka. Uso wake mzuri ulibadilika ghafla.
Dakika kumi baadaye, Lisa alilikuta gari la rangi nyeusi la Alvin kando ya barabara. Alipoingia ndani ya gari, alitazama huku na huko kama mwizi.
“Kwanini una wasiwasi, unaogopa kwamba Kelvin atatuona?” Alvin alishika sigara katikati ya vidole huku mkono wake ukiwekwa kwenye usukani. Katikati ya moshi huo uso wake mzuri ulionyesha hali ya kejeli.
Kwa wakati huu, Lisa alimchukia sana. “Bwana Kimaro, si unakumbuka uliingia ukumbini na mpenzi wako na mama mkwe mtarajiwa sasa hivi? Sasa kila mtu anajua kuwa wewe ni mtu wa Melanie. Mtu akiniona nikiingia kwenye gari lako, anaweza kudhani kwamba ninakutongoza.”
“Una wivu?” Macho makali ya Alvin yalikuwa yakimtazama.
“Siwezi kuwa na wivu kuhusu hilo.” Lisa alidhihaki na kujibu kwa sauti ya kuchafukwa. “Kwa nini unataka kukutana nami? Ikiwa hakuna kitu kikubwa, niache niondoke sasa.” Alifanya kana kwamba alilazimishwa kuwa hapo.
Alvin alikuwa na msongo wa mawazo sana wakati huo kuhusu Kelvin. Aliamua kupasua kero iliyokuwa ndani yake moja kwa moja. Alimshika mkono na kumdhihaki, akisema, “Sasa Kelvin amerudi, hujisikii kuniona tena, sih? Lisa, ukiendelea kuwa na tabia ya kipuuzi mbele yangu, nitakufukuza wewe na Kelvin kutoka Nairobi.”
“Inatosha.” Lisa alichoka kabisa na maneno yake. Macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira. “Ulinidhalilisha sana wakati wa sherehe sasa hivi, labda utaniacha tu baada ya mimi kujiua."
“Utajiua kweli? Kwa mwanamke kama wewe, uko tayari kujiua?" Alvin alibana shavu lake kwa mkono wake wa kushoto. Maneno yaliyotoka kwenye mdomo wake yalikuwa ya kikatili kuliko hapo awali.
Macho ya Lisa yalijawa na chuki. “Nakuchukia, Alvin. Wewe ndiye mwanaume mpumbavu zaidi niliyewahi kukutana naye.”
“Thubutu kusema tena.” Alvin kweli alipoteza utulivu sasa. Alimshika koo, uso wake ukionyesha sura ya ukatili.
“Nimekosea kusema hivyo? Unavutiwa na mwanamke kama Melanie. Wewe ni kipofu, sivyo?” Lisa akapiga kelele, "Familia ya Mahewa ina nia mbaya, lakini unaendelea kuwatetea. Unawasaidia tu na kuwaunga mkono. Wakati wowote ninapokumbuka jinsi nilivyopenda mtu kama wewe wakati huo, ninachukizwa sana.”
“Ha! Ulikuwa unanipenda?” Alvin alijifanya kana kwamba anasikia mzaha. "Usipotoshe neno 'upendo'."
Lisa alijidharau kutamka hivyo na kutoa tabasamu la uchungu.
“Lisa, usijaribu kunichokoza. Najua vizuri kile kilicho mawazoni mwako.” Macho ya Alvin yalikuwa makali. “Kadiri ninavyoishi, hutaweza kuishinda familia ya Mahewa. Nina na Joel hawataweza kutalikiana.”
Lisa alimpa macho ya kifo. Kutokana na hasira kali, kifua chake kilihisi uzito asioweza kuubeba.
Alvin akaisogeza sigara kwenye midomo yake na kuutoa ule moshi taratibu. Moshi huo ulifunika uso wake ambao ulitoa hisia ngumu. "Isipokuwa, nimpatie mwanamke mwingine mimba, sitafikiria kumwacha Melanie." Alipomaliza kusema tu, alifungua vifungo vya shati lake chini ya kola. Kisha akatazama nje ya dirisha. Hiki kilikuwa tayari kidokezo kikubwa cha uvumilivu ambao angeweza kumpa. Ilikuwa pia nafasi yake ya mwisho kwake.
Lisa alipigwa na butwaa. Aliona kidogo inamchanganya. Alimaanisha nini? Je, alikuwa akimaanisha kwamba alitaka atafute mwanamke wa kumpa mimba, au yeye ndiyo achukue mimba yake?Hata hivyo, Lisa alihisi maumivu makali sana kufikiria kitu ambacho Alvin alipanga kufanya na mwanamke mwingine.
“Nimekuelewa. Naweza kuondoka sasa hivi?” Baada ya mapambano ya kukata tamaa, hatimaye Lisa alikata tamaa.
Sura ya: 174
“Umeelewa nini?” Aliuliza kwa dharau Alvin. "Naelewa. Unataka kusema kwamba huwezi kuachana na Melanie, sivyo? Tabasamu la uchungu liliruka usoni mwa Lisa. “Ikiwa ndivyo ilivyo, hupaswi kuwa pamoja nami pia.”
Alvin alishindwa cha kusema. Mwanamke huyo kwa kawaida alikuwa na akili sana. Nini kilikuwa kimetokea kwenye ubongo wake sasa? Hakuweza kuwa na wasiwasi juu yake. Hapo hapo akanyoosha mguu na kukanya moto hadi mwisho, akaondoka kwa kasi kama yote.
Gari ilisafiri moja kwa moja hadi kitongoji cha Oasis. Alvin alimburuta Lisa hadi juu ya ghorofa na kumsukuma kuelekea kwenye kochi. Akiwa amechemka kwa hasira, alisema, “Lisa, unataka niweke mambo wazi zaidi, sivyo? Nataka uachane na Kelvin mara moja. Unaruhusiwa kuwa na mimba ya mtoto wangu tu. Ikiwa utabeba mimba, nitaachana na Melanie.”
Lisa alikodoa macho. Alijifanya kana kwamba amepigwa na radi. Kwa muda mrefu, alibakia ameganda kama kaota mizizi mahali hapo.
Alvin akavua suti yake na kuitupa chini. Aliiweka mikono yake nyuma ya kichwa chake na kumweka juu ya kifua chake. “Lisa, wewe ni jeuri. Hiki ni kikomo cha uvumilivu wangu na pia nafasi yako pekee.”
Lisa alishikwa na mshangao, na akili yake ilikuwa imefika mwisho wa kufikiri. Hakuweza kuelewa nia yake, kwa kuzingatia kwamba alimchukia sana na hata alimuona mchafu wakati huo, sasa angeachana na Melanie maadamu angebeba mimba ya mtoto wake? Je! ni kwa sababu bado alikuwa na hisia kwake…?
Moyo wake ulianza kudunda. Wakati huo, alihisi kushawishika. Tayari alikuwa akijua kwamba kifo cha Sheryl kilihusishwa na familia ya Mahewa. Zaidi ya hayo, kwa kuwa Farres alikuwa amejaribu kumuua mara moja, ilikuwa inawezekana kwamba angejaribu kufanya hivyo tena. Njia pekee ya mkato ya kuzuia hilo lisitokee ilikuwa ni kumtegemea Alvin.
Baada ya kuona hali yake ya kushtuka, Alvin alimbeba na kuelekea chumbani. Baada ya kumuweka juu ya kitanda, alimkandamiza kwa kasi na kumbusu. Muda si muda Lisa alijitambua na kumsukuma. "Hapana. Siwezi kufanya hivi.”
Alvin alimtazama kwa macho mekundu. “Kwa nini?”
Moyo wa Lisa ulimuuma, akakwepa macho yake. “Mimi ni mchumba wa Kelvin. Ikizingatiwa kuwa amejinyima mengi kwa ajili yangu, siwezi kumuumiza. Ingawa nataka kulipiza kisasi, sitaki kutumiwa kama chombo ili kulipiza kisasi.”
Damu ya Alvin taratibu ikawa barafu. Alimtazama kwa huzuni kwa kile kilichoonekana kama mshangao wa kukata tamaa. Ghafla, alitoa kicheko dhaifu. “Potelea mbali.” Ghafla alimsukuma hadi sakafuni huku hewa ya uadui ikitoka kwenye uso wake. Lisa huku akiyazuia machozi yake, alivaa nguo zake haraka na kutoka nje ya chumba hicho.
“Lisa, hii ndiyo nafasi ya mwisho ninayokupa. Utajuta.” Alvin alimtazama kama shetani. Baada ya kutetemeka, Lisa aliondoka Oasis bila kugeuza kichwa chake.
Alirudi nyumbani kwa Ngosha akiwa na wasiwasi, akagundua kuwa vitu vyote vya chumbani kwake vilikuwa vimetupwa nje na vimetawanyika kwenye nyasi. Nina na Melanie walisimama mlangoni kwa kuridhika. “Toa vitu vyako na upotee. Haukaribishwi hapa.”
Lisa alikunja ngumi. “Hii ni nyumba ya baba yangu. Huna haki ya kunifukuza.”
“Utani ulioje. Mimi ni mke halali wa Joel. Nyumba hii kwa kiasi fulani ni mali yangu. Huwezi kuendelea kukaa hapa bila kibali changu.”
Nina alionyesha mtazamo wa kiburi. “Ulifikiri unaweza kumfanya Joel anitaliki kwa sababu ya ile ajali ndogo? Endelea kuota."
Lisa akatoa simu yake kumpigia Joel. Simu iliunganishwa, lakini hakuna aliyejibu.
“Acha kupiga simu. Mzee Ngosha anamsomesha Joel kwa sasa,” Nina alimdhihaki, “Huoni? Mzee Ngosha amekubaliana na wazo la kukufukuza pia, kwa hivyo hakuna kitu Joel anaweza kufanya juu yake.”
“Umesikia? Fanya haraka upotee basi.” Melanie hata alipiga teke nguo zake zilizoanguka chini.
Lisa alipunguza hasira yake na kuingiza vitu vyake kwenye sanduku lake kimoja baada ya kingine. Ni yeye tu aliyejua jinsi alivyokuwa na hasira ndani ya moyo wake. Angewalipa kwa kumdhalilisha mapema au baadaye.
Hata hivyo, kabla Lisa hajaweka vitu vyake vyote, Melanie alichukua maji machafu na kummwagia moja kwa moja. Vitu vyake vyote vikalowa kabisa.
“Lo, samahani. Nilikuwa napanga tu kumwaga maji machafu pembeni bahati mbaya nikakumwagia.”
Melanie alipokuwa akifurahia hali yake, Lisa alidhihaki. "Sasa unajishaua kwa kuridhika kwa sababu tu unaungwa mkono na familia ya Kimaro. Lakini umewahi kufikiria kuwa Alvin anaweza kukuacha siku moja?"
Usemi wa Melanie ulibadilika sana. “Wewe ni bullsh*t nini? Alvin atanioa hivi karibuni.”
"Natumai." Lisa aliuma mdomo kwa kejeli. Kwa kuzingatia kwamba Alvin alikuwa ameeleza wazi nia yake ya kurudiana naye muda si mrefu, alifikiri kwamba hakuwa na hisia na Melanie.
Lisa alipomaliza tu kuongea alibeba vitu vyake na kuondoka bila kuwapa Nina na Melanie nafasi ya kuendelea kumdhihaki. Kwa kuwa hakuwa na mahali pa kukaa Nairobi, hakuwa na budi ila kukaa katika hoteli ya nyota tano iliyokuwa karibu.
Usiku Joel alimpigia simu kwa haraka. "Lisa, kwanini umetoka nyumbani?"
“Baba, hujui kwamba nimefukuzwa?”
"Nini?" Joel alipandwa na hasira. "Damn, Nina ni mtu mbaya sana! Nitashughulika naye. Uko wapi? Ngoja nije nikuchukue sasa hivi.”
"Hakuna haja. Nitakaa nje kwa muda huu,” Lisa alijibu kinyonge, “Sasa kwa kuwa Nina na Melanie wana Alvin Kimaro akiwaunga mkono, ninaogopa hawatakujali. Zaidi ya hayo, Babu anachukua upande wao pia. Nikirudi nyumbani, badala yake niitakuwa vurugu.”
Joel aliendelea kujilaumu. "Ni bure kwangu kukuacha ukiteseka, Lisa."
“Usijali, baba. Hii ni ya muda tu. Ninaamini kila kitu kitakuwa sawa,” Lisa alijibu kwa huzuni huku akitazama nje ya dirisha.
Siku inayofuata, baada ya kuamshwa na simu yake, Lisa alikimbilia kwenye chumba cha mikutano ofisini. Meneja Mkuu Ngololo alisema kwa wasiwasi, "Mwenyekiti Jones, ingawa shamba la Nairobi limeidhinishwa, tuna matatizo na leseni ya kuanzisha biashara huko Kenya."
"Ulijaribu kutumia njia za chinichini?" Lisa akasugua nyusi zake.
“Ndiyo, lakini imeonekana kutozaa matunda.” Meneja Mkuu Ngololo alilazimisha tabasamu. “Hapo awali tulikubaliana. Lakini ghafla walibadilisha mawazo yao. Walisema kuna mzozo juu ya ardhi yetu na kiwanja kilicho jirani yetu.”
Meneja Lomeo kutoka idara ya uhandisi aliuliza, "Je, tumemkosea mtu yeyote huko Nairobi, Mwenyekiti Jones?"
Sura ya:175
Lisa alikumbuka jinsi Alvin alivyozungumza wakati anaondoka jana yake. Alihisi likuwa ni kazi yake. Meneja Mkuu Ngololo aliongeza, “Vilevile kampuni ya KIM international wameondoa hisa zao zote ghafla kutoka kwenye mtaji wa kampuni. Mtaji wetu sasa unayumba. Ikiwa hatutapata pesa za kunyanyua mtaji haraka iwezekanavyo, mnyororo wetu wa biashara utakatika na kampuni yetu itaachwa juu ya kuti kavu. Ikiwa ni hivyo, kampuni inaweza kufilisika.”
Lisa alishangaa sana lakini hakuwa na haja ya kuilaumu KIM International. “Nitatafuta njia ya kutokea,” Lisa alisita kabla hajajibu.
Baada ya kikao kumalizika, alienda ofisini kumpigia Alvin na kugundua kuwa alikuwa ameifungia namba yake. Alitoa kicheko cha uchungu. Inavyoonekana, alikuwa amemkosea. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kumuomba Joel msaada.
Baada ya Joeli kuulizia jambo hilo aliona ni ajabu. “Lisa, umemkosea nani? Hata mimi nimeshindwa kukusaidia wakati huu. Nina hakika hii haihusiki na familia ya Mahewa.”
“Sijui hata ni nani nimemkosea. Ngoja nijaribu kukumbuka.” Lisa alikata simu akiwa ameduwaa. Aliingiwa na wazo la kumwomba Joel kuwekeza mtaji katika kampuni ili kutatua suala la mtaji wa kufanyia kazi, lakini alikumbuka kampuni ya Ngosha haikuwa ya Joel pekee. Kuwekeza zaidi ya makumi ya mabilioni ya shilingi kungehitaji idhini ya Mzee Ngosha. Hata hivyo, Mzee Ngosha bila shaka angekataa ombi hilo.
Kwa bahati nzuri, Chris Maganga aliingia ofisini na kuwasiliana na Lisa mchana ule kwa njia ya video. Alikuwa amesikia mwenendo mbaya wa kampuni. "Lisa, nimesikitishwa na kitendo cha cha KIM International kuondoa hisa zao ghafla na kuathiri mtaji wa kampuni. Hapa kuna shilingi bilioni hamsini naongeza kama hisa zangu kwenye mtaji wa kuendeshea biashara za kampuni. Zinaweza kuwa na uwezo wa kusaidia kampuni kwa wakati huu.”
“Mjomba Chris, asante sana!” Lisa aliguswa. Katika hali kama hiyo, kila mkurugenzi mwingine alikuwa akikosoa tu mambo na kujitetea. Hawakuwa tayari kuchangia pesa yoyote.
"Mama yako aliijenga kampuni hii kwa uchungu. Sitaki kuiona ikifungwa.” Chris akashusha pumzi ndefu. "Hata hivyo, umegundua nini juu ya kifo cha mama yako?"
Baada ya kufikiria kidogo, Lisa alijibu, “Nadhani kifo cha mama yangu hakina uhusiano wowote na familia ya Mahewa. Niligongana na Farres hapo awali na hakuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya tukio la kujaribu kuniua kwa ajali ya gari. Lakini nilipotaja kifo cha mama yangu, alionekana kushangaa kana kwamba haelewi chochote.”
“Hiyo ni ajabu. Kabla ya mama yako kufariki, simu yake ya mwisho ilitoka Nairobi.” Chris alihisi kuchanganyikiwa. "Kuna mtu mwingine basi nyuma ya tukio."
Lisa alisugua chake ake. Akili yake ilikuwa imechanganyikiwa. Chris aliweza kujua kwamba alikuwa amechoka. Baada ya muda, alisema kwa huruma, “Mfadhaiko unaoupata sasa ni mwingi sana kwako katika umri huu mdogo. Ikiwa huwezi kuishughulikia, rudi tu Dar es Salaam. Sawa?”
Lisa alikuwa katika butwaa. Nyakati fulani, alihisi kwamba hakupaswa kwenda Nairobi hata kidogo. Hapo awali, alifikiri kwamba uhusiano wake na baba yake ungeboreka, jambo ambalo lingemwezesha kupata ushindi hatua kwa hatua. Lakini, familia ya Mahewa ilitegemea familia ya Kimaro ambayo waliitegemea kama msaada wao mkubwa. Kweli, alikuwa amechoka!
Alikuwa akishughulikia mgogoro huo siku kadhaa zilizofuata lakini, pande husika zilikataa kukutana naye. Alipotoka nje ya ofisi ya ardhi, alikutana na Jack Kimaro. Jack alipigwa na butwaa kumuona. Alionekana kuwa hakuwa amelala vizuri siku chache zilizopita.
“Unaonekana umechoka, Bi Jones, unakabiliwa na shida yoyote?" Jack aliuliza huku akitabasamu. Muonekano wake ulikuwa tofauti na Alvin. Alvin alikuwa na dharau, kiburi na kujisikia. Kwa kulinganisha, kulikuwa na haiba ya umaridadi juu ya Jack. Jack alikuwa na sifa laini, na alionekana mpole alipotabasamu.
“Ndiyo. Kuna tatizo kuhusu ardhi ya kampuni yangu.” Lisa aliitikia kwa unyonge.
Jack aliinua kichwa chake kwa mshangao. “Ninaelewana na kamishna wa ardhi hapa. Labda naweza kukusaidia?”
Lisa alipigwa na butwaa. Hakuwa amepanga kumuomba msaada. Baada ya yote, alikuwa sehemu ya familia ya Kimaro, kwa hivyo, alionekana kuachwa njia panda.
"Hata hivyo niikikusaidia, basi utaniwia fadhila." Jack alimkonyeza huku akitabasamu.
Lisa alilazimisha tabasamu. "Kwa kuzingatia hali yangu ya chini, huenda nisiweze kurudisha fadhila, Bwana Kimaro."
"Inategemeana. Kwa kuzingatia kwamba uliweza kuweka utulivu wako hata ulipokaribia kufa, nadhani unaweza kuahidi." Jack ghafla alimtazama na kutabasamu. “Ninaelewa jinsi unavyohisi hivi sasa. Hali yetu ni sawa. Katika familia ya Kimaro, watu kila mara huniita mwana haramu ambaye niliharibu familia ya Alvin na baba yake.”
Lisa alipigwa na butwaa. Kwa kweli hakumpenda Jack wakati huo, lakini, wote wawili walikuwa katika hali sawa sasa. “Hupaswi kuhangaika kuhusu hilo, bwana Kimaro. Hatukupata kuchagua asili zetu. Zaidi ya hayo, maisha yako ni ya furaha zaidi kuliko yangu. Wazazi wako wameoana.”
“Ndiyo. Hata hivyo, watu wengine huwa wananilinganisha na kaka yangu. Siku zote ninaishi katika kivuli chake.” Jack alieleza kwa masikitiko. "Njoo, nitakupeleka kwa kamishna."
“… Asante, Bwana Kimaro.”
Lisa alimfuata baada ya kusita kwa muda. Ikizingatiwa kuwa kulikuwa na wafanyikazi zaidi ya 10,000 katika kampuni yake waliotegemea maisha yao kupitia ajira za kampuni hiyo, asingeweza kuachia nafasi hiyo ya kuikomboa kampuni.
Siku tatu baadaye, Alvin alirejea Nairobi baada ya mkutano wake nje ya nchi kumalizika. Mara tu ndege ilipotua kwenye uwanja wa ndege, Hans alimripotia kuhusu hali ya kampuni. Alvin alisikiza kimya kimya. Baada ya kuingia ndani ya gari, Hans alimwambia kwa umbea, "Mgogoro wa leseni ya ardhi ya Mawenzi umetatuliwa."
Alvin akavua tai shingoni. “Nani alimsaidia?”
"Jack Kimaro." Hans alitoboa siri.
Kulikuwa na muda wa ukimya. Hans alihisi woga alipogundua kwamba Alvin alikuwa akikunja mdomo wake maridadi. "Jack anapanga kufanya nini?"
"Labda ni kwa sababu Jack amegundua kuwa una uhusiano na Lisa?" Hans aliuliza kwa mashaka.
“Nadhani amekuwa mvivu sana siku hizi. Mradi wa kiwanda chetu k huko Sudani Kusini unasuasua. Nitampeleka huko ashughulikie,” Alvin alisema kwa huzuni.
Hans aliingiwa na huruma. "Suala la usalama katika Sudan Kusini limekuwa na utata sana hivi karibuni, huko si salama sana. Bibi Kimaro anaweza kukasirishwa na hilo.”
"Atakwenda atake asitake." Kwa kutojali kabisa, Alvin alicheka. "Kwa hiyo, Lisa ana matumaini kwamba Mawenzi iko salama na anaweza kuishi maisha yake bila wasiwasi? Kwa bahati mbaya, ana pointi nyingi dhaifu.”
Akiwa amekunja uso wake, Hans alihisi kwamba Alvin alikuwa akipandisha wazimu. Kwa kumwondoa Jack Kimaro, kungezuka ghasia kubwa ndani ya KIM international wakati palikuwa shwari kabisa kipindi hayupo.
Siku ambayo ujenzi katika ardhi ya Mawenzi huko Nairobi ulipoanza, Lisa alimpigia simu Jack kwa njia ya whatsapp baada kumkos kwenye simu ya kawaida. “Asante kwa msaada wako mapema, Bwana Kimaro. Ningependa kukukirimu kwa chakula kama ishara ya shukrani yangu.”
"Sitaweza kuungana nawe Lisa." Jack alitoa kicheko cha uchungu. “Nimefika Jubah leo. Kaka yangu aliniagiza kuja Sudan Kusini kufuatilia mradi fulani.”
Lisa alishtuka. “Lakini nilisikia Sudan Kusini kwa sasa iko kwenye fujo. Kuna mzozo unaoendelea kati ya maeneo ya kusini na kaskazini mwa nchi. Wageni wengi huwa wanajiingiza kwenye matatizo makubwa huko. Inawezekanaje Alvin akakufanya uende huko?"
Jack alinyamaza kwa dakika moja kisha akajibu, “Hata mimi sina uhakika sana. Ghafla alipandwa na hasira, lakini hata hivyo, hiyo sio kawaida. Nadhani amekuwa akinichukia kwa muda mrefu sana.”
Lisa alihisi kurusha matusi. Alijua kwa hakika kwamba Alvin alikuwa amegundua kwamba Jack alimsaidia.
“Usijali. Mama yangu atapata njia ya kunirudisha haraka iwezekanavyo,” Jack alisema kwa uchungu.
“Sawa. Nitakuandalia chakula ukirudi basi.” Lisa akakata simu.
Usiku, Kelvin alimpeleka kwenye mkahawa wa kichaga ulioko Nairobi kwa chakula cha jioni. Kelvin hakusema neno katika safari yote. Haijalishi Lisa alikuwa mwepesi kiasi gani, aliweza kuhisi kwamba hakuwa na furaha. "Nini tatizo? Nani amekukera?”
“Ulihama nyumbani kwa baba yako na kukaa hotelini peke yako bila kunitaarifu. Hukunifahamisha kuhusu tatizo katika kampuni yako pia.” Kelvin alikunja uso kwa hasira. “Lisa, mimi ni mchumba wako, lakini mbona unanichukulia kama mtu wa pembeni?”
Lisa alisita kwa muda na kusema, “Una mambo mengi ya kushughulikia katika kampuni yako pia. Sikutaka kukusumbua na matatizo yangu—”
"Bila kujali idadi ya mambo yanayoendelea katika kampuni yangu, ninaweza kuyashughulikia. Kwa kuwa wewe ni mpenzi wangu, ni jukumu langu kukusaidia kadri niwezavyo. Je, wanaume hawatakiwi kushiriki mzigo wa wanawake wao?” Kelvin alikuwa na sura ya kuchukiza kuliko Lisa alivyowahi kumuona. “Najua sina nguvu katika sehemu kama Nairobi, lakini nataka ujue kwamba haijalishi nini kitatokea, nitafanya niwezavyo kukusaidia. Lisa, unanifanya nijione sifai sana.”
“Samahani.” Lisa aliomba msamaha. “Sitafanya hivyo tena.”
"Ikiwa kweli umemaanisha kuomba msamaha, hama kwenye hoteli na uje ukae nami." Kelvin alimshika mkono. "Nimenunua jumba la kifahari hapa Nairobi, ambalo ni sawa kwa sisi sote kukaa."
Lisa alipinga wazo hilo bila kujua. Awali alimsababisha apoteze figo kwa sababu alikuwa akimkinga na hatari ya kifo, sasa hakutaka kumsababishia kupoteza kabisa maisha yake......ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.