JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP.........................0628924768
SEHEMU YA......................................140
Sura ya 140
“Bwana Kimaro, kifungua kinywa chako kimefika.” Shangazi Linda alitoka na kifungua kinywa alichotengeneza.
Alvin akakitazama, na uso wake ukachukizwa mara moja. "Lisa Jones, kwanini hukuniandalia kiamsha kinywa?"
"Wewe ndio ulisema chakula changu ni kichafu kama mimi." Lisa alimtazama kwa utulivu. Siku zote alikuwa hivi. Alipomuelewa vibaya, alimdhalilisha kwa kumwambia chakula chake ni kichafu na asimpikie tena, lakini sasa alitaka apike tena. Je, hakuchoka kumnyanyasa?
"Nitengenezee sasa hivi." Uso wa Alvin ulikuwa mbaya kwa hasira.
"Hapana. Mimi siyo yaya wako.” Lisa alisimama baada ya kumaliza uji wake. "Naenda kazini."
Alvin aligeuka na kuongea na Shani aliyekuwa amesimama mlangoni. “Mfuate kwa karibu. Akithubutu kwenda hospitali, mpige na umrudishe hapa.”
"Mimi sio mtumwa wako." Macho ya Lisa yalikua mekundu kwa hasira. Tayari alikuwa ameamua kutokwenda hospitali, lakini bado alisisitiza kumlazimisha kumwekea mlinzi wa kumchunga. "Alvin Kimaro, usiende mbali sana."
“Kwa kuwa ulinichanganya, unapaswa kuwa tayari kuwa mtumwa wangu. Hakuna anayeweza kwenda kinyume na mimi.” Alvin hakujieleza sana, lakini maneno yake yalitosha kudhihirisha hasira zake.
Lisa alichukua mkoba wake na kuondoka huku Shani akimfuata.
Njiani kuelekea ofisini kwake, haijalishi Lisa aliendesha gari kwa haraka vipi, Shani alikuwa makini naye muda wote. Kwenye maegesho, Lisa alishuka kwenye gari na Shani akamfuata kwa nyuma kwa kasi.
“Shani, unaweza kuacha kunifuata? Sitaenda hospitalini.” Lisa alitmwambia Shani kwa upole. Kwa kweli, hakuwa na shida yoyote na mlinzi yule.
"Samahani, hili ni agizo la Bwana Kimaro, bosi wangu."
“Agizo ni la Alvin, lakini usalama ni wa kwangu. Najua namna ya kujilinda mwenyewe!” Lisa mwishowe alikasirika. “ Sawa, Alvin alikuajiri? Anakulipa kiasi gani? Mimi nitakupa mara mbili." Lisa akatoa kadi kwenye begi lake.
Shani hakujali. “Bi Jones, haijalishi unanipa kiasi gani. Nilifunzwa na familia ya Kimaro. Ninafanya kazi kwa ajili yao tu.” Lisa alipigwa na butwaa. Je, familia ya Kimaro ilikuwa na watu wengi kama Shani? Familia ya Kimaro ilionekana kuwa na mambo mengi zaidi kuliko vile alivyofikiria. “Kwa hiyo lazima umekuwa na Alvin kwa muda mrefu. Kwa maana hiyo unamjua mtu anayeitwa Sarah?”
Hali ya wasiwasi ikaangaza kwenye macho tulivu ya Shani. Ingawa lilitoweka hapo hapo, Lisa bado aliliona vizuri. “Nilimsikia Alvin akimzungumzia siku moja akiwa amelewa. Lazima awe mpenzi wake wa zamani. Walikuwa wanapendana sana?"
“Bi Jones, hayo yote ni ya zamani. Bwana Kimaro ana wewe tu moyoni mwake sasa,” Shani alisema haraka.
"Ndio hivyo?" Lisa alitabasamu kwa kujidharau. Alikuwa akimpima tu Shani, lakini jibu la Shani lilimhakikishia kwamba kweli Alvin alikuwa na mpenzi wa zamani anayeitwa Sarah. Alimwita jina lake wakati alikuwa amelewa. Je, iliwezekanaje kuwa Lisa ndiye pekee moyoni mwake sasa?
“Shani, asante kwa kuniambia hivi.” Aligeuka na kwenda juu ofisini.
Shani alimfuata kinyonge.
•••
Siku iliyofuata, saa kumi na nusu jioni, Pamela alitoka hospitali baada ya kumtembelea Kelvin, akihisi huruma moyoni mwake.
Kama asingekuwa amekosea na kumchanganya Alvin na Kelvin hapo mwanzo, huenda Lisa na Kelvin wangekuwa tayari wameoana. Hapo Kelvin asingepoteza figo pia. Hata hivyo, haikufaa kujutia juu ya maziwa yaliyokwishamwagika sasa.
Akatoa simu yake na kumpigia Patrick. “Patrick, unakwenda kuwachukua wazazi wangu, au unaenda moja kwa moja kwenye Mgahawa tuliokubaliana kukutana?”
“Niko na mkutano ofisini ambao unaweza kuendelea hadi saa kumi na moja na nusu. Nitaenda huko moja kwa moja baadaye. Nisaidie kuomba radhi kwa wazazi wako kwa ajili yangu,” Patrick alisema kwa sauti ya upole.
“Ni sawa, lakini usichelewe. Baba yangu anachukia watu ambao hawatimizi ahadi zao.” Pamela alimuonya kwa upole.
“Usijali, ni suala la maisha yangu. Hakika sitachelewa. Tayari nimekuandalia zawadi ambayo wazazi wako watapenda. Tutafunga ndoa mapema, nami nitakuwa mumeo.” Patrick akatabasamu kwa dhati. Moyo wa Pamela ulikuwa mtamu alipokuwa akimsikiliza.
Baada ya kukata simu, Pamela aliendesha gari kuwachukua wazazi wake kisha akaenda Mambo Garden Restaurant. Ilikuwa saakumi na moja kamili jioni alipofika. Baada ya kuagiza chakula, kaka yake Forrest alifika. Saa kumi na mbili jioni bado Patrick alikuwa hajafika. Babake Pamela alikosa subira, akasema, “Kwa nini bado hajafika? Si sawa kutufanya wazee tungojee.”
Pamela alisema, “Baba, ni saa za jioni sasa. Pengine kuna msongamano mkubwa wa magari barabarani.”
Mama yake aliitikia kwa kichwa na kukubali. “Wafanyabiashara wana mambo mengi ya kushughulikiwa mwishoni mwa mwaka, hiyo inaeleweka. Kuwa na subira zaidi.”
Pamela alimpigia simu Patrick, lakini hakupokea, akajifariji. "Lazima asipokee kwa sababu yuko barabarani, atakuwa karibu tu hapa."
Baada ya nusu saa nyingine, Patrick hakutokea tu. Baba yake alikasirika. “Ni mara yake ya kwanza kukutana nasi lakini anatuletea dharau namna hii. Hata ukimpigia simu ni bure. Sidhani kama yeye ni mkweli hata kidogo. Sitakubali kukuruhusu uolewe naye.”
Wakati huu, mama yake hakusema chochote, na Forrest pia alikuwa na uso wa kukata tamaa. “Achana naye. Sio kama hakuna wanaume wengine ulimwenguni."
Pamela alihudhunika. Mbele ya shutuma za familia yake, alijilazimisha kutotoa machozi. Yeye tu alijisikia kukata tamaa sana kwa aibu. Zamani, alimuahidi mara nyingi, lakini sasa, hata alikosa mkutano wa kwanza pamoja na wazazi wake. Je, alimpenda kweli?
Mama yake akasema. “Pamela, jambo la muhimu zaidi katika maisha ya mwanamke ni kupata mwanaume ambaye ni mzuri kwako kwa moyo wote. Bado wewe ni mdogo, kwa hivyo usikimbilie kuolewa. Sasa, tule. Chakula kinakuwa baridi.” Wakati wote wa chakula, ilikuwa kama anatafuna nta. Mpaka mwisho, Patrick hakutokea, wala hakupiga simu hata mara moja kuelezea shida ni nini.
Baada ya kuachana na familia yake, Pamela aliendesha gari hadi ofisini kwa Patrick. Ofisi yake ilikuwa tayari imefungwa. Alianza kuhisi wasiwasi kidogo. Alikuwa na wasiwasi kwamba huenda Patrick alikuwa amepata ajali ya gari au kitu kibaya. Hata hivyo, hakujua namba za wazazi wa Patrick. Baada ya kusita kwa muda, alimpigia simu Linda. Hakutarajia kuwa mtu aliyemjibu angekuwa ni mwanamume ambaye sauti yake aliifahamu vizuri. “Habari, Pamela…”
Pamela alitazama sura yake iliyokuwa na ukungu kwenye dirisha la kioo mbele yake na ghafla akacheka peke yake. Je, alionekana kama mjinga? “Kwa nini hukupokea nilipokupigia simu? Na mbona unapokea simu ya Linda?”
“Pamela, samahani. Linda alipata ajali ya gari jioni. Niko hospitalini sasa. Nilisahau kabisa hata kuchukua simu yangu ofisini,” Patrick alisema kwa hatia, “Oh, nimechelewa sana? Mmemaliza kula? Tafadhali mwambie baba na mama smahani kwa kushindwa kuja.
Nitawaalika kwenye chakula cha jioni wakati mwingine.”
"Hakuna haja tena," Pamela alisema kwa sauti isiyo na maana.
"Pamela, ilikuwa ni dharura wakati huu ..."
“Ndiyo, kila kitu kuhusu Linda ni dharura. Kwani amekufa? Kilema? Kwani hana wazazi tena, ana wewe tu?"
Moyo wa Patrick ukasisimka. "Pamela, unawezaje kusema maneno kama haya? Kwani Linda alitaka kupata ajali? Hata kama humpendi, unapaswa angalau umuonee huruma.”
Pamela alidhihaki. “Sawa, nimekuuliza swali. Kwani amekufa? Amepooza? Mlemavu?”.........ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
